Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Kitila Mkumbo amesema aliyekuwa mgombea wa urais wa Chadema, Edward Lowassa, hana budi kukubali matokeo licha ya kupoteza nafasi hiyo.
Pia
Profesa Mkumbo alisema mgombea huyo kisheria, hakuwa na haki ya
kujitangaza mshindi wa nafasi ya urais katika uchaguzi wa mwaka huu.
Juzi,
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilitangaza matokeo ya kura za urais
zilipopingwa Jumapili, Oktoba 25 mwaka huu na kumtangaza mgombea wa
urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli mshindi, lakini Lowassa siku
hiyo pia alisema ameshinda katika uchaguzi kwa kura 10,268,795 sawa na
asilimia 62 na kuitaka tume hiyo kumtangaza mshindi.
Profesa
Mkumbo ambaye pia alipendekezwa na chama cha ACT- Wazalendo kugombea
nafasi hiyo na kukataa, alisema Lowassa aliingia kwenye kinyang’anyoro
hicho akifahamu kuwa tume ndiyo yenye mamlaka ya kumtangaza mshindi.
Alisema licha ya mchuano mkali kati yake na mgombea wa CCM anatakiwa kukubali matokeo.
“Hivyo
Lowassa na wenzake wa Ukawa hawana msingi wowote wa kisheria au
kisiasa kutangaza ushindi wenyewe. Walikubali kushiriki katika uchaguzi
huu wakati wakifahamu kikamilifu kuwa NEC ndiyo yenye jukumu la
kutangaza mshindi na mshindwa katika uchaguzi.”
Aliongeza: “Zaidi ya hayo, takwimu za uchaguzi zinaeleza pia.”
Hata
hivyo alisema katika uchaguzi huu ambao ni wa kihistoria kutokana na
upinzania mkali kati ya CCM na upinzani tofauti na miaka ya nyuma, bado
upinzani umepoteza nafasi ya ubunge licha ya kujinyakulia viti 76 huku
CCM ikiwa na viti 188.
“Kupoteza viti hivyo ni ishara kwamba ushindi wa Lowassa haukuwa wa uhakika,”alisema Profesa Mkumbo na kuongeza;
“...nawashauri
Ukawa kukubali kwamba Dk Magufuli ndiye rais mtaule wa awamu ya tano.
Wahakikishe wanashirikiana na kufanya kazi naye kazi kwa karibu katika
kipindi chake cha miaka mitano ya uongozi. Kwa namna hiyo wataweza kuwa
chachu ya kupata Katiba Mpya itakayowezesha kubadili mazingira ya
kikatiba na kisheria katika uchaguzi ujao.”
~Mpekuzi blog
Post a Comment