Rais Mteule Dk John Magufuli ameamua kufunguka kuhusu ugumu aliokabiliana nao wakati wa mchakato wa kampeni akieleza kuwa uchaguzi wa mwaka huu umekuwa na changamoto kubwa kutokana na hujuma zilizofanywa na wanafiki waliojificha ndani ya Chama cha Mapinduzi(CCM).
Amesema
amekerwa na hali hiyo kiasi cha kushindwa kuvumilia kuizungumzia jana,
hasa baada ya kuona uchaguzi umekwisha, hivyo ni vyema wanafiki hao
wakajisalimisha kwa kutubu kwa kuwa wamekigharimu chama hicho na
kusababisha kiwe kwenye wakati mgumu.
Amesema
kwamba asiposema atakuwa ni mnafiki kwa sababu uchaguzi umekwisha bora
wawekwe wazi kwa sababu anaona ni bora kuishi na mchawi kuliko mnafiki,
alimuomba Mwenyekiti wa chama hicho Jakaya asiwahurumie wanaokihujumu,
hivyo kusababisha washindwe kufika kwenye malengo.
“Nisiposema
nitakuwa mnafiki msema kweli ni mpenzi wa Mungu watubu wajirekebishe ni
mara kumi kuwa na mpinzani kutoka nje kuliko ndani ya chama,mipango
yenu mtaipanga mchana usiku wataitoa nje ni afadhali uwe na mchawi
atakuroga ufe kuliko mnafiki ndani, ” amesema Maguli katika hafla ndongo ya kumpongeza baada ya kukabidhiwa cheti na kuongeza:
“
Lakini ukweli utabaki kuwa ukweli wewe ni mwenyekiti lakini ulikaa na
wanafiki ndani ya CCM, ndiyo wametufanya wakati mwingine tufike hapa
tulipofika, ndiyo wametufanya tufike hapa tulipo , leo kwa hiyo nakuomba
ukitengeneze chama chetu vizuri ukishamgundua mnafiki usikae naye
fukuza kesho, nimeona hili nilizungumze lakini unisamehe sana kwa sababu
ningebaki nalo moyoni ningenisababishia kiungulia,ambacho nimekiona
wakati nazunguka nikiwa kwenye kampeni,”
Kuanza kazi haraka
Magufuli
amewahakikishia wananchi kuwa mara baada ya kuapishwa siku hiyo hiyo
atanza kufanya kazi, kwa kuwa hakuomba nafasi hiyo kwa majaribio bali
kuwatumikia wananchi kwa dhati.
Pia
ameomba ushirikiano mzuri kutoka kwa wananchi ili waweze kufanikisha
yale ambayo wameahidi wakati wa kampeni yeye na na Makamu Rais Samia
Suluhu Hassan, ili waweze kutimiza wajibu wa kuwatumikia bila kinyongo
na kuyatimiza yake waliyoahidi wakati wa kampeni.
“Kwa
hiyo niwaombe ndugu zangu watanzania wote bila kujali vyama vyetu
tunaomba sana ushirikiano wenu , tusipopata ushirikiano wetu hatuwezi
kuyatimiza kwa wakati, tisipopata ushirikiano mzuri kutoka kwenye
mtatuchelewesha mara unataka kufanya hizi mara kuna maandamano
yakashindwe, yakalegee yakabaki huko huko yalikoanzia, kwa sababu sisi
tunataka tufanye kazi,” alisema Dk Magufuli na kushangiliwa.
Aliongeza kusema“
Katika kuzunguka kwetu kwa wananchi wameona kuna kero nyingi za maji,
umeme, miundombinu, wananchi wanataka zitatuliwe haraka, niwaombe
watanzania bila kujali vyama naomba ushirikiano wenu mzurI, ili
tufanikishe hayo tuliyoahidi wakati wa kampeni,” alisisitiza.
Amsifu JK
Rais
huyo Mteule alimsifu Rais wa awamu ya nne Dk Jakaya Kikwete akisema
kwamba ni wa tofauti kwani licha ya kumtembeza katika maeneo karibu yote
ya Ikulu , lakini pia amekuwa na busara za kukubali na kuendeleza
madaraka ya kupokezana.
“
Nataka niseme mheshimiwa Rais una moyo wa pekee, Mungu akujalie sana
viongozi wengi Afrika wanapokaribia kuondoka madarakani wengine huwa
wanatengeneza hata katiba tofauti ili katiba ili waendelee kubaki
madarakani, lakini wewe upo tayari kuondoka hata leo,” alisema.
Dk
Magufuli alisema anaamini kwamba wananchi wataendelea kumuombea,
kumlinda kwa kuwa amethamini Tanzania Kwanza, hivyo ataendelea kuhitaji
busara zake pale itakapobidi atakapoingia madarakani.
Awali
akitoa maoni yake mara baada ya Dk Magufuli kukabidhiwa cheti cha
ushindi, Mratibu wa Taifa wa ULINGO, Dk Ave Maria Semakafu alisema
anaamini wanawake wengi wamefurahishwa na ushindi huo kwa sababu kwa
umewezesha pia kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi kuwa na Makamu
wa Rais mwanamke Samia Suluhu Hassan.
“
Tumefungua ukurasa mpya kwani miaka 20 ya tamko la Mkutano wa wanawake
Duniani wa mwaka 1995 Beijing, tumekuwa na mrejesho mzuri kuhusu
mwitikio wa Serikali kuweka ushiriki sawa wa nafasi za uongozi badala ya
kuwafanya wanawake wawe watu wa kupiga kura kwa kuchagua viongozi wa
ngazi mbalimbali lakini sasa nao wanachaguliwa, wanaaminika na kupewa
nafasi kubwa ya uongozi kama hii,” alisema Dk Semakafu .
Alisema
uchaguzi wa mwaka huu umekuwa ni wa kihistoria katika mambo mengi licha
ya ushindani wa kisiasa lakini wanawake wawili walikuwa ni wagombea
akiwamo Anna Mgwira aliyekuwa akigombea nafasi ya urais kupitia chama
cha ACT Wazalendo.
“
Binafsi nilikuwa nafuatilia kwa karibu kampeni zao kulikuwa na mwitikio
mkubwa wa watu walikuwa wakiwasikiliza na hakukuwa na hali ya
udhalilishaji wa kuona kwamba hawastahili kwa sababu tu wao ni wanawake
,” alisema .
Post a Comment