
Dorine akiwa hospitali baada ya kuchomwa mikono na shangazi yake.
Katika tukio hilo la Septemba 26, mwaka huu, Scola alidaiwa
kutekeleza tendo hilo, chanzo kikielezwa ni upotevu wa shilingi
20,000.Kwa mujibu wa chanzo makini, Scola alimtaka Dorine aseme
amezipeleka wapi fedha hizo, lakini binti huyo alisema hajui chochote.Ilidaiwa kwamba, katika hali isiyokuwa ya kibinadamu, wakati Dorine akiwa anahojiwa tayari maji ya moto yalikuwa yakichemka.Ilisemekana kwamba, baada ya kuona Dorine hataki kusema zilipo fedha hizo, Scola akamuamuru aingize mikono ndani ya sufuria lililokuwa jikoni huku maji yakichemka.
Dorine alipokataa, Scola akadaiwa kumshika kwa nguvu, akisaidiana na mama yake ambaye ni bibi wa Dorine na kuizamisha kwenye sufuria la maji mikono hiyo na kumsababishia mtoto huyo majeraha ya kutisha.
Ilisemekana kwamba, baada ya tukio hilo, familia hiyo ilifanya siri kubwa na kutompeleka hospitalini lakini baadhi ya majirani walibaini hilo na kusambaza taarifa ndipo familia hiyo ikampeleka hospitalini kwa siri.

....Akisaidiwa na nesi kuinuka.
Alipofikishwa katika Hospitali ya Kanisa Katoliki Luguruni, Mbezi
mtoto huyo alilazwa baada ya mahojiano na wauguzi ambapo aliwaeleza kila
kilichotokea.Hata hivyo, maelezo ya Dorine kwamba aliunguzwa na
shangazi na bibi yake yalipingwa na Scola ambaye alisema mtoto huyo
alikuwa akikimbia akaangukia maji ya moto.Taarifa alizopata mwanahabari wetu kwenye hospitali hiyo kupitia muuguzi wa zamu, zilieleza kuwa taarifa sahihi za tukio hilo ni zile alizozitoa mtoto huyo.Katika mahojiano na wauguzi, Dorine ambaye alikuwa amelazwa kwenye Chumba cha Stuff Na. 16 hospitalini hapo, alifafanua kuwa anaishi kwa shangazi yake baada ya baba yake mzazi kuachana na mama yake na baba kuoa mwanamke mwingine.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili ulibaini kwamba, Scola alishikiliwa na Jeshi Polisi Kituo cha Mbezi-Kwayusuf na baadaye aliachiwa kwa dhamana lakini bibi hakukamatwa.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, RPC Camilius Wambura alipoulizwa na gazeti hili juu ya tukio hilo alikiri kulijua na kwamba alipokea taarifa za aina mbili hivyo alimwagiza OCD wa Mbezi-Kwayusuf kulifuatilia na kumpa taarifa kamili.
Alisema taarifa moja ilidai, Dorine aliunguzwa lakini ya pili ilidai aliangukia kwenye sufuria yenye maji ya moto hivyo uchunguzi unaendelea ili kupata taarifa kamili.


Post a Comment