
VYAMA vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vimesitisha kampeni zake ngazi zote ili kutoa fursa kwa wananchi kuaga mwili wa aliyekuwa mwenyekiti mwenza, Dk. Emmanuel Makaidi.
Dk.
Makaidi, aliyekuwa pia Mwenyekiti wa National League for Democracy
(NLD) alichokianzisha mwaka 1992, na mgombea ubunge jimbo la Masasi
mkoani Mtwara, alifariki dunia Alhamisi wiki iliyopita katika hospitali
ya Nyangao, Masasi, baada ya kuugua ghafla ugonjwa wa shinikizo la damu
(presha).
Ofisa
Habari wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tumaini Makene,
akizungumza kwa niaba ya UKAWA, jana jijini Dar es Salaam, alisema
usitishaji wa kampeni umelenga kuonesha heshima ya kipekee kwa Dk.
Makaidi ambaye alijitoa muhanga katika kuimarisha UKAWA kwa hali na
mali.
“Kesho
(Leo) kuanzia saa tatu asubuhi tutakuwa viwanja vya Karimjee kwaajili
ya kutoa heshima za mwisho kwa Dk. Makaidi, sambamba na hilo pia
tutasitisha kampeni zetu za ngazi zote na katika shughuli hiyo viongozi
wote wa kitaifa wa UKAWA pamoja mgombea Urais watakuwepo” alisema Makene.
Baada
ya mwili wa Dk. Makaidi kuagwa katika viwanja vya Karimjee, shughuli ya
mazishi ya mwanasiasa huyo mkongwe aliyefariki akiwa na umri wa miaka
74 itahitimishwa katika makaburi ya Sinza jijini Dar es Salaam.
Ratiba
ya kampeni itaendelea Jumatano ya tarehe 21 Oktoba kwa mgombea urais wa
Ukawa, Edward Lowassa kwenda mkoani Morogoro kumalizia majimbo ambayo
hakufika katika awamu yake ya kwanza ya kampeni mkoani hapo.
Majimbo hayo ni pamoja na jimbo la Kilombero, Mlimba, Mikumi, Ulanga Mashariki na Ulanga Magharibi.

Post a Comment