Hatimaye aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema anayeungwa mkono na vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa, Edward Lowassa ametangaza kurudi nyuma na kujipanga upya kwa awamu ya pili.
Akiongea juzi
kwenye tafrija fupi ya kuishukuru timu yake ya kampeni pamoja na
wananchi waliomuunga mkono, Lowassa aliwataka wote waliokuwa wanamuunga
mkono kutokata tamaa na kujipanga upya kwani awamu ya pili inakuja.
Lowassa
alieleza kuwa kilichofanyika ni sawa na kuichelewesha bahati ya mtu na
kudai kuwa anachelewesha bahati ya mtu hawezi kuiondoa bali ataizuia kwa
muda tu.
“Unaweza kuchelewesha bahati ya mtu, lakini hauwezi kuiondoa,”
alisema Lowassa na kuisihi timu yake kushikamana na kujipanga upya.
Muda wote aliokuwa akiongea timu yake hiyo pamoja na viongozi wa Ukawa
walionekana kumuunga mkono na kumshangilia.
Lowassa
alipinga matokeo yaliyokuwa yanatangazwa na NEC yaliyompa ushindi Dkt.
John Magufuli na kuwasilisha pingamizi lake kwa Tume hiyo akiwataka
kusitisha mchakato wa utangazaji wa matokeo lakini haikuwezekana.
Aliituhumu Tume hiyo kwa kile alichodai kumpokonya ushindi wake na kutangaza matokeo batili kwa kumpunguzia kura na kumuongezea Dkt. Magufuli.
Aliituhumu Tume hiyo kwa kile alichodai kumpokonya ushindi wake na kutangaza matokeo batili kwa kumpunguzia kura na kumuongezea Dkt. Magufuli.
Alidai
kuwa baada ya kufanya majumuisho ya kura kwenye vituo vyote, yeye
alipata kura zaidi ya milioni 10 tofauti na idadi ya kura milioni 6
iliyotangazwa na Tume hiyo.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alieleza kuwa kwa
kuwa matokeo ya urais hayawezi kupingwa mahakamani, hivi sasa hawana
jinsi zaidi ya kurudi nyuma na kujipanga upya kwa ajili ya awamu ya
pili.
Alisema hivi sasa watafungua kesi za majimbo 30 ya ubunge ambayo wana ushahidi kuwa yalipokonywa kibabe na CCM.
Katika
hatua nyingine, Mbowe alieleza kuwa hivi sasa viongozi wa Ukawa kwa
pamoja wamepanga kupiga kambi visiwani Zanzibar kuanzia wiki ijayo ili
kumuongezea nguvu mgombea urais kupitia CUF, Maalim Seif Shari hamad ili
wananchi wasipokonywe haki yao kwa kufutwa matokeo ya uchaguzi
wanayoamini kuwa yanampa ushindi mgombea huyo wa CUF.
Post a Comment