Featured

Loading...


Raisi mstaafu,Jakaya Mrisho Kikwete Aingia Mtaani.....Afanya 'Shopping’ Mlimani City

Kwa mara ya kwanza tangu aondoke madarakani mwanzoni mwa mwezi huu, jana Rais Jakaya Kikwete alionekana akifanya manunuzi katika maduka yaliyopo jengo la Mlimani City, jijini Dar es Salaam.

Kikwete, ambaye alikuwa amevalia suti maarufu kama ‘kaunda suti’ yenye rangi nyeusi, alionekana akiingia katika viunga vya Mlimani City saa 5:00.

Mwandishi wetu ambaye alikuwepo katika viunga hivyo vya Mlimani City alishuhudia Kikwete akiwasili katika maeneo hayo akiwa katika msafara wa magari manne na pikipiki moja.

Rais huyo mstaafu pia alikuwa ameambatana na mkewe, Salma Kikwete, aliyekuwa amevalia mavazi ya kitenge pamoja na walinzi wao wanne.

Hatua hiyo ilionekana kushangaza baadhi ya watu waliokuwepo katika maeneo hayo, huku wengi wao wakionekana kutaka kumsalimia.

Mwandishi wetu ambaye  muda wote alikuwa akimfuatilia Rais Kikwete na mke wake, alishuhudia wakiingia katika maduka ya Game na kufanya manunuzi kwa dakika zisizopungua 10 hadi 15 na  baadaye kutoka nje na walinzi wake wakionekana kubeba mifuko iliyokuwa na bidhaa walizonunua.

Kama ilivyo hulka ya Rais Kikwete alipotoka nje ya duka hilo alianza kusalimiana na mtu mmoja ambaye alionekana kufahamiana naye.

Hatua hiyo ilimpa fursa ya kuwasalimia watu wengine waliokuwa karibu na tawi la benki moja.

Baada ya hapo msafara wake uliondoka na kuelekea Barabara ya Sam Nujoma.

Tangu achaguliwe kuwa rais mwaka 2005 itifaki na majukumu yake ya urais yalikuwa yakimbana Rais Kikwete na hivyo kushindwa mambo yake binafsi kama walivyo raia wengine.

Pamoja na kwamba Kikwete sasa ni raia, lakini kutokana na wadhifa aliowahi kuushika wa urais bado halingani na raia wengine wa kawaida, ingawaje majukumu ya urais yamepungua na hivyo kumpa fursa ya kutembea katika maeneo ya wazi na kufanya matumizi ya kawaida kama alivyofanya jana.

Tangu alipoachia kiti cha urais na kumkabidhi Dk. John Magufuli baada ya kuapishwa Novemba 5, Kikwete amekuwa akiishi nyumbani kwake Msoga, mkoani Pwani.

Rais Kikwete aliondoka rasmi Ikulu na familia yake Ijumaa iliyopita Novemba 6 na kuanza maisha mapya kijijini kwake huko.

TOA MAONI YAKO HPO CHN1 KUHUSU HABARI HII

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright JICHO LETU
Back To Top