Featured

Loading...


Wabunge Wateule Waitwa Dar Katika Hafla ya Kuapishwa Dk. Magufuli.


Ofisi Ndogo ya Bunge jijini Dar es Salaam, imewataka wabunge wote wateule walioko majimboni kufika katika ofisi hizo Jumatano wiki hii kwa ajili ya kushiriki hafla ya kuapishwa kwa Rais Mteule itakayofanyika Novemba 5, mwaka huu katika Uwanja wa Uhuru.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel, alisema wabunge wateule watakaohudhuria hafla hiyo wanatakiwa kuja na vyeti vya kuteuliwa walivyopewa na Wasimamizi wa Uchaguzi.

“Kila Mbunge mtarajiwa, atatakiwa kuwasilisha cheti kwa Maofisa wa Bunge wakati wa mchakato wa usajili  na kitambulisho kingine chochote kinachotolewa na mamlaka inayotambulika na kinachomtambulisha jina lake kamili kama linavyoonekana kwenye cheti cha uteuzi wa ubunge,” alisisitiza.

Aidha, alisema mchakato wa usajili wa wabunge wateule utafanyika katika viwanja  vya Bunge la 11 na kuongeza wabunge hao watajitegemea usafiri wa kuelekea bungeni.

Joel alisema mkutano huo utaanza siku ambayo Rais Mteule atakapoitisha Bunge.

Alisema siku hiyo shughuli mbalimbali zitafanyika zikiwamo za uchaguzi na kiapo kwa Spika, viapo vya wabunge, uthibitisho wa jina la Waziri Mkuu, uchaguzi wa Naibu Spika na ufunguzi rasmi wa Bunge la 11.

Alivikumbusha vyama  vya siasa vyenye usajili wa kudumu vinavyotaka kusimamisha mgombea wa nafasi ya Spika vianze mchakato wa kupata mgombea katika ngazi ya vyama baada ya tangazo kutolewa na kuwasilisha jina lake kwa Katibu wa Bunge.

Alivisistiza vyama kuzingatia kuwa mgombea wa nafasi hiyo anaweza kuwa mbunge au mwanachama yeyote wa chama hicho kwa masharti kwamba siyo mbunge mteule.

Hali kadhalika, alisema vyama vya siasa vinatakiwa kuwasilisha jina la mgombea Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) siku tano kabla ya uchaguzi kujiridhisha kwamba mgombea ana sifa za kuwa mbunge.
~Mpekuzi blog

TOA MAONI YAKO HPO CHN1 KUHUSU HABARI HII

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright JICHO LETU
Back To Top