Featured

Loading...


Vigogo Watatu wa TRA Akiwemo Tiagi Masamaki Waachiwa Kwa Dhamana Baada ya Kutimiza Masharti


Hatimaye vigogo watatu wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) akiwemo kamishna wa forodha na ushuru wa mamlaka hiyo, Tiagi Masamaki wameachiwa  kwa dhamana na mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, baada ya kutimiza masharti ya dhamana yaliyotolewa mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam.
 
Washtakiwa hao wamedhaminiwa kwa sh. Bilioni 6.6, na hati za mali zisizohamishika zilizowasilishwa katika mahakama ya Kisutu ambapo dhamana ya vigogo hao imetolewa na hakimu mkuu mfawidhi wa mahakama ya Kisutu, baada ya washtakiwa kutimiza masharti ya dhamana yaliyotolewa na jaji wa mahakama kuu Winfrida Koroso.

Jaji Koroso alisema ili washtakiwa wawe nje kwa dhamana kila mwombaji alitakiwa aweke mahakamani sh. Bilioni 2.1 au hati za mali isiyohamishika zenye thamani hiyo na wadhamini wawili watakaosaini dhamana ya sh. Milioni 20.

Baada ya hati hizo kuwasilishwa mahakamani hapo, hakimu alikubaliana na hati hizo na kuwapatia washtakiwa dhamana, lakini wakili wa serikali Christopher Msigwa aliomba mahakama hati hizo zikafanyiwe  uhakiki kwa sababu zingine anamashaka nazo.

Aidha wakili Msigwa amedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na itatajwa Desemba 30 mwaka huu.

Washtakiwa ambao hawajaomba dhamana na wamerudishwa rumande na mahakama kuu ni msimamizi mkuu wa ICD-Azam, Eliachi Mrema, mchambuzi mwandamizi wa masuala ya biashara TRA, Khamis Omary, Haroun Mpande wa kitengo cha mawasiliano ya kompyuta ICT - TRA, meneja uendeshaji usalama na ulinzi wa Azam ICD, Raymond Louis na meneja Azam ICD, Ashraf Khan.

Desemba 3, mwaka huu, Masamaki na wenzake walipandishwa kizimbani katika mahakama ya Kisutu, wakikabiliwa na mashitaka ya kula njama ya kudanganya na kuisababishia serikali hasara ya sh. Bilioni 12.7 kutokana na makontena 329 kukwepa kodi.

TOA MAONI YAKO HPO CHN1 KUHUSU HABARI HII

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright JICHO LETU
Back To Top