Waziri
wa zamani wa Mamboya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe
amekaribishwa kujiunga na Chama Cga Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
ikiwa ni siku chache tangu atoe maoni yake akiikosoa serikali ya Rais
John Magufuli.
Mwanasiasa
huyo mkongwe amekaribishwa na Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya
Kinondoni, Boniface Jacob ambaye alimshawishi kwa kutumia mifano ya
wanasiasa wakongwe waliokuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliohamia
Chadema na Ukawa kwa ujumla akiwemo Edward Lowassa, Frederick Sumaye na
Kingunge Ngombale Mwiru.
Wiki
iliyopita Membe alinukuliwa akimkosoa Dk Magufuli katika maeneo kadhaa,
likiwamo la kubana matumizi, kudhibiti safari za nje na uteuzi wa
Baraza la Mawaziri.
Jana,
meya huyo kutoka Chadema alisema watu wanamshangaa Membe na
kumshambulia siyo kwa sababu amesema mambo ya ajabu, ila yeye si mtu
sahihi wa kutoa kauli hiyo.
“Watu
hawashangai alichosema (Membe) kwa sababu siyo hoja ngeni, zimesemwa
sana na wapinzani. Wanachoshangaa ni yeye (Membe) kusema hayo. Hafanani
na hoja anazoziongea,” alisema.
Jacob
ambaye alikuwa diwani katika manispaa hiyo katika Serikali ya Awamu ya
Nne alisema, hoja zilizotolewa na Membe ni nzuri na kama zingetolewa na
mpinzani zingeonekana zina mashiko zaidi.
"Asiwe
vuguvugu, hicho ndicho kinachompa shida. Kama anataka kuja huku asiwe
na wasiwasi chama changu kitampokea na hata hayo anayoyaongea yatakuwa
na mantiki na watu watamsikiliza kwa sababu ni upinzani,” alisema na kuongeza;
“Avuke
moja kwa moja kama walivyofanya akina Kingunge (Ngombale Mwiru),
(Edward) Lowassa, na (Frederick) Sumaye kuhamia upinzani.”
Jacob
alisema Sumaye na Lowassa ambao waliwahi kuwa mawaziri wakuu na
Kingunge aliyekuwa kada mkongwe wa CCM, walikuwa viongozi wa ngazi za
juu, lakini walihamia upande wa pili (upinzani) na sasa wanaisimamia na
kuikosa Serikali kwa uhuru.
“Asiwe mwoga kwamba ataishi maisha gani, Sumaye na Lowassa wamekuwa mawaziri wakuu wakaondoka na maisha yanaendelea.”
Hata
hivyo, Jacob alisema Membe hakupaswa kukosoa sera ya Rais Magufuli ya
matumizi na Rais kudhibiti safari za nje, kwa sababu yeye amenufaika
nayo.
“Nadhani
hakuwa mtu sahihi kusema hayo, alipaswa kwanza kumtafuta mtu mwingine
aseme halafu yeye afuate baadaye, lakini kuanza kusema yeye moja kwa
moja wakati alikuwa ananufaika na anachopinga Rais, anaonekana anamwonea
wivu na mgongano wa masilahi.
“Sasa
anapoanza yeye kujibu inashangaza. Kwa sababu yeye alikuwa Waziri wa
Mambo ya Nje, iliyokuwa inafanya matumizi makubwa halafu unakosoa
unaonekana kabisa unaonyesha kuna mgongano wa masilahi,” alisema na kuongeza:
Jacob alisema kwa mpinzani kusema hivyo angeonekana anataka kumuwajibisha Rais ili hayo mambo yaangaliwe kwa kina zaidi.
Alitoa
mfano wa waziri wa zamani, Dk Makongoro Mahanga na kusema alipoikosa
Serikali hakushambuliwa kwa sababu alishahama kutoka CCM na sasa yupo
upinzani.
“Alipozungumzia suala la matumizi ya ardhi, Serikali haikujibu ilikaa kimya kwa sababu aliyeongea ni mtu sahihi,” alisema na kuongeza.
"
Kwanza alikuwa kwenye Baraza la Mawaziri na pili hivi sasa yupo kwenye
upande wa kuishambulia na kuikosoa Serikali na kuiwajibisha.”
Post a Comment