Kikao
cha pili cha Bunge la kumi na moja linalotarajiwa kuwa na ushindani
mkali wa hoja kati ya wabunge wa vya upinzani vinavyounda Ukawa na
wabunge wa CCM kimeanza leo mjini Dodoma huku mambo 8 muhimu
yakitarajiwa kuibua mjadala mkubwa.
Jambo la kwanza ni
kujadili hotuba ya Rais John Magufuli aliyoitoa bungeni hapo mwaka jana
katika kikao cha kwanza cha bunge hilo. Hapo suala la kupambana na
ufisadi linatarajia kuleta hoja nzito zaidi kutoka kila upande. Hotuba
ya Rais ilisifiwa na takribani kila mwananchi pamoja na wanasiasa
mbalimbali.
Pili, Kurudiwa kwa uchaguzi Mkuu wa Zanzibar. Hili ni suala nyeti na linalopaswa kubebwa kwa uangalifu mkubwa.
Wabunge
wa Ukawa na CCM wanatarajiwa kurusha makombora yao ya hoja na maoni
katika kusaidia namna ya kupata muafaka. Bila shaka hapo mengi yataibuka
na huenda kukawa na mgongano mkubwa wa hoja na mawazo.
Tatu,
Zoezi la Bomoabomoa pia linaweza kupewa nafasi yake katika Bunge hilo
hususan katika utekelezaji wake na mapungufu yaliyojitokeza.
Nne,Maazimio
ya Bunge juu ya sakata la ESCROW linaweza kuwa mada moto zaidi katika
bunge hilo kwani tayari kumekuwa na vutankuvute kabla ya Bunge.
Mbunge
wa jimbo la Ubungo Saed Kubenea na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe
ambao ni mahasimu wa kisiasa wameonekana kuwa na nia moja katika
kulirudisha bungeni sakata la ESCROW. Mmiliki wa Kampuni ya IPTL/PAP,
Harbinder Singh Sethi amepinga mahakamani kurudishwa bungeni kwa sakata
hilo lakini Zitto amesisitiza kuwa mtu binafsi hawezi kulizuia Bunge
kutekeleza majukumu yake.
Tano,Utekelezaji
wa sera ya elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha nne pia
ni suala ambalo litaleta mjadala katika Bunge hilo, kwa kuzingatia
changamoto zilizoanza kuripotiwa.
Sita,Uteuzi
wa wajumbe wa kamati za Bunge ambao vyama vya upinzani vinavyounda
Ukawa vimeulalamikia na hata kutishia kuususia unatarajiwa kuwa sehemu
ya hoja zitakazoleta mjadala mkubwa katika Bunge hilo.
Saba,Ni
migogoro iliyoibuka katika chaguzi za Mameya wa majini na Manispaa
pamoja na wenyeviti wa Halmashauri. Waziri wa TAMISEMI atakuwa na kazi
ya kujibu hoja na maswali yatakayokuwa yanaelekezwa kwake kuhusu zoezi
hilo.
Nane, Hoja
binafsi za wabunge zinatarajiwa kuibuliwa na kuleta mjadala mzito kwani
tayari baadhi ya wabunge wamekwisha eleza nia yao ya kupeleka bungeni
hoja binafsi kuhusu masuala mbalimbali.
Bunge
hili linatarajiwa kuwa la kipekee na lenye changamoto kubwa kwa kuwa
na idadi kubwa ya vijana na idadi kubwa ya wabunge wa upinzani ambao
wameunda umoja wao.
Post a Comment