Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Viwanda la
Umoja wa Mataifa UNIDO lenye makamo makuu yake Nchini Vienna Ausria Bw.
Li Yong walipokuta katika Ofisi za Umoja wa Afrika (AU) Addis Ababa
leo Januari 31,2016, Makamu wa Rais yupo Nchini Addis Ababa Ethiopia
kumuwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za
Afrika unaojadili kuhusu masuala ya Usalama Barani Afrika.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akizungumza na Ujumbe wa Shirika la Maendeleo la Viwanda la Umoja wa
Mataifa lenye Makao Makuu yake Nchini Vienna Austria uliongozwa na
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Bw. Li Yong, leo Januari 31,2016 kwenye
Ofisi za Umoja wa Afrika (AU) Addis Ababa, katika mazungumzo yao
Viongozi hao walizungumzia juu ya kuendeleza ushirikiano kwenye
maendeleo ya Viwanda utakaotolewa na UNIDO kwa Serikali ya Tanzania ili
kuifanya Tanzania iwe Nchi ya Viwanda kuanzia mwaka 2015/2020, ambapo
Mkurugenzi huyo ameahidi kuitembelea Tanzania wakati wowote kuanzia
sasa. Makamu wa Rais yupo Nchini Addis Ababa Ethiopia kumuwakilisha Rais
John Magufuli kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika unaojadili
kuhusu masuala ya Usalama Barani Afrika.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Viwanda la Umoja wa Mataifa UNIDO lenye
makamo makuu yake Nchini Vienna Ausria Bw. Li Yong akisisitiza jampo
kwa Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan walipokuta katika Ofisi za
Umoja wa Afrika (AU) Addis Ababa leo Januari 31,2016.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akipokea taarifa yenye mipango ya Maendeleo ya Viwanda kutoka kwa
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda la Umoja wa Mataifa
Bw. Li Yong baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao yaliyofanyika leo
Januari 31,2016 katika Ofisi za Umoja wa Afrika (AU) Addis Ababa,
Makamu wa Rais yupo Nchini Addis Ababa Ethiopia kumuwakilisha Rais John
Magufuli kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika unaojadili kuhusu
masuala ya Usalama Barani Afrika.
Post a Comment