Siku moja baada ya kifo cha rubani Rodgers Gower (37) aliyekuwa anaendesha helikopta inayomilikiwa na Mwiba Holdings, baadhi vyombo vya habari vya kimataifa vimeripoti kuwa huenda bunduki iliyomuua ni ile iliyokuwa inatumika kuulia tembo.
Miongoni
mwa vyombo hivyo ni magazeti ya Uingereza ya Daily Mail, The Guardian,
The Sun, The Telegram, The Independent, Shirika la Habari la Ufaransa
AFP na Shirika la Utangazaji la Marekani CNN.
Mbali
na vyombo hivyo, jana asubuhi mwili huo ulifanyiwa uchunguzi ambao
ulionyesha matundu manne ya risasi, moja kwenye mguu, mawili begani na
jingine kwenye paji la uso ambako risasi iliingilia kichwani na haikuwa
imetoka.
Chanzo cha habari katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru, ulikopelekwa mwili huo kilisema walipewa maagizo kuhakikisha hauondolewi hadi risasi iliyopo kichwani imeondolewa.
Chanzo cha habari katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru, ulikopelekwa mwili huo kilisema walipewa maagizo kuhakikisha hauondolewi hadi risasi iliyopo kichwani imeondolewa.
“Unajua
huyu aliyefariki ni Mzungu, hata kama amefanyiwa postmoterm hapa
anaweza kufanyiwa nyingine Aga Khan, Dar es Salaam na akifikishwa kwao
Uingereza anafanyiwa tena, ndivyo walivyo wenzetu,” alisema.
Ijumaa
iliyopita, Gower aliuawa kwa risasi wakati akiendesha helikopta hiyo
kwenye doria dhidi ya majangili katika Pori la Akiba la Maswa, mkoani
Simiyu akiwa pamoja na raia wa Afrika Kusini, Nicky Bester ambaye
alinusurika kifo.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe alisema Serikali
inaendelea na uchunguzi ili kuwabaini majangili waliohusika.
Alivyouawa
Daily Mail lilisema jana kuwa inawezekana hata bunduki iliyomuua Gower ni ile waliyokuwa wanatumia majangili hao kuua tembo. Lilieleza kuwa wakati Gower akiwa katika doria, aliona mabaki ya tembo wawili chini.
Alivyouawa
Daily Mail lilisema jana kuwa inawezekana hata bunduki iliyomuua Gower ni ile waliyokuwa wanatumia majangili hao kuua tembo. Lilieleza kuwa wakati Gower akiwa katika doria, aliona mabaki ya tembo wawili chini.
Gazeti
hilo lilimnukuu Pra tik Patel, mmoja wa marafiki wa karibu marehemu,
akisema wakati anaendelea na doria aliona tembo mwingine ambaye hakuwa
ameuawa muda mrefu.
“Baada
ya kuona hivyo, akataka ageuze ili wakamwangalie yule tembo, huku
akijaribu kuona kama kuna majangili, ndipo mwanamume mmoja alitokea
akiwa na bunduki na kupiga kwenye uvungu wa helikopta,” alisema Patel ambaye pia ni mfanyakazi mwenzake.
“Ile
risasi ilitoboa uvungu wa helikopta na kupenya ndani, ikampiga rubani
kwenye mguu na sehemu ya bega na uso kisha kutoboa paa la helikopta na
kutoka nje … kutokana na uzito wa silaha iliyotumika kumuua, pengine
ndiyo ileile ambayo majangili walitumia kuua tembo.”
Hata hivyo, gazeti la The Telegram, lilieleza kuwa bunduki iliyotumika kumuua Gower ni AK47.
“Alipokuwa
anamkaribia tembo mmoja aliyeuawa, ndipo akapigwa risasi na kufariki
kabla ya timu ya waokoaji kufika katika eneo hilo,” ilisema sehemu ya habari hiyo.
Mwanzilishi
wa Mfuko wa Hifadhi wa Friedkin (FCF) aliyetoa taarifa kwa vyombo vya
habari, Dan Friedkin ambaye aliwahi kufanya kazi na Gower alisema ni
jambo la kusikitisha kuona rubani huyo, aliyekuwa katika operesheni ya
kusaidia Tanzania kupambana na majangili ameuawa na haohao majangili.
The
Guardian liliripoti kuwa jukumu kubwa la marehemu ambaye pia alikuwa
mhasibu kitaaluma, lilikuwa kusafirisha watalii kwenye kambi mbalimbali
za hifadhi.
Gower
ambaye pia alihitimu masomo ya urubani wa helikopta mwaka 2004 London,
Uingereza amekuwa akifanya doria kwa kushirikiana na wahifadhi kwa ajili
ya kupambana na majangili kwenye hifadhi.
Akizungumzia mipango ya mazishi, Patel alisema jana kuwa suala hilo bado linajadiliwa na familia ya marehemu.
Hata hivyo, taarifa nyingine zilieleza kuwa mwili huo unatarajiwa kusafirishwa kwenda Uingereza kwa mazishi.
Chanzo
cha kuaminika katika Mount Meru kilisema muda mfupi baada ya mwili huo
kufikishwa, wakala wa kusafirisha miili ya raia wa kigeni alifika na
kuzungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Mwiba Holdings, iliyokuwa
inamiliki helikopta hiyo.
Post a Comment