Jengo refu lilojengwa chini ya kiwango lililopo katika mtaa wa Indiraghandi jijini Dar,kama lionekanavyo pichani.
WAZIRI
wa Nyumba, Ardhi na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amewaagiza
watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na Shirika la Nyumba la
Taifa kubomoa jengo refu lilojengwa chini ya kiwango lililopo katika
mtaa wa Indira Ghandhi ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa.
Lukuvi
ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam kabla ya kuelekea kwenye ziara
fupi katika Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani ambapo nako pia amebaini
matatizo mbalimbali katika sekta ya Ardhi.
“Miezi
sita iliyopita Rais Mstaafu alikuja hapa akaagiza jengo hili libomolewe
na nyie mkajiridhisha kweli lafaa kubomolewa sasa inakuwaje mpaka leo
linaendelea kuwepo? Naagiza mfanye haraka jengo hili ndani ya mwezi
mmoja taratibu za ubomoaji ziwe zimeanza ili kulinusuru taifa kuingia
katika janga jingine.”alisema Waziri Lukuvi.
Akiwa
bagamoyo waziri Lukuvi alibaini katika Wilaya ya Bagamoyo upotevu wa
viwanja vya wanachi ambavyo walitakiwa kupewa katika eneo la ukuni
ambapo vimetoweka
Mara
baada ya kupata taaarifa hiyo mmoja wa wakaazi wa bagamoyo ambaye
alitoa malalamiko juu ya viwanja hivyo mbele ya mkutano wa hadhara na
kutaja kuwa Halmashauri ilichukua kiasi cha pesa kuanzia laki sita kwa
kila mtu mwaka 2005 na kuahaidi kuwapatia viwanja lakini mpaka leo
hawajapewa.
Mara
baada ya kupata taarifa hiyo waziri Lukuvi aliwagiza watendaji wa
wilaya hiyo ndani ya miezi sita wawe wamewapatia wakazi hao viwanja
hivyo.
Sehemu ya jengo ambayo inaonekana imepasuka.Picha na Emmanue Massaka
Post a Comment