Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano sehemu ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga amesema daraja la Kigamboni litaanza kutumika kuanzia Machi mwaka huu.
Akizungumza
mara baada ya kukagua hatua za ujenzi wa daraja hilo Eng. Nyamhanga
amemtaka msimamizi wa ujenzi huo kuhakikisha hatua ya ujenzi iliyobaki
inakamilika katikati ya mwezi februari na kuanza kazi mwanzoni mwa mwezi
Machi.
“Hakikisheni
Machi mosi magari yaanze kupita rasmi kwenye daraja hili na hivyo
kufungua ukurasa mpya kwa wakazi wa Kigamboni ambao kwa muda mrefu
wamekuwa wakikabiliwa na msongamano katika eneo la Magogoni”, amesema Eng. Nyamhanga.
Eng.
Nyamhanga amesisitiza kuwa Serikali inaangalia uwezekano wa kuunganisha
daraja la Kigamboni na barabara ya Charambe,Mlandizi hadi Chalinze ili
kupunguza msongamano wa magari katikati ya Jiji.
Amemtaka
meneja wa mradi wa ujenzi wa daraja hilo toka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii
(NSSF), Eng. John Msemo kuhakikisha anatafuta Wakala makini
atakayesimamia na kuendesha mradi huo.
Daraja
la Kigamboni lenye urefu wa mita 680, unasimamiwa na Mfuko wa Hifadhi
ya Jamii (NSSF), Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Wizara ya
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano linatarajiwa kuishi zaidi ya miaka 100 na
kuwa na uwezo wa kupitisha mizigo ya tani 56 zinazokubalika katika nchi
za jumuiya ya madola.
IMETOLEWA NA ;
KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO
WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO.
KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO
WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO.
Post a Comment