WAENDASHA pikipiki 100 wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga wametakiwa kuacha kuchukulia mambo ya siasa katika mafunzo wanayopewa na wataalamu wa usalama barabarani kwa vile elimu wanayoipata iatawasaidia katika kujikinga na ajali zisizokuwa za lazima.
Hayo yalisemwa jana na Diwani wa Kata ya Kahama Mjini, Abas Omary alipofunga mafunzo ya siku mbili ya bodaboda yaliyotolewa na wataalamu kutoka Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT), Dare es Salaam.
Alisema mafunzo hayo ni kwa manufaa ya waendesha pikipiki na si wanasiasa hivyo ni bora wanaposikia kuna mafunzo kujitokeza kwa wingi hali ambayo itachangia kupata elimu sahihi ya kuhusu usalama barabarani.
“Ninawaomba bodaboda mnaposikia kuna mafunzo ya usalama barabarani ni bora mkajitokeza kwa wingi kwa sababu katika mafunzo haya lengo ni kutoa elimu kwa watu zaidi ya 200 lakini kwa sasa ni madereva 100 ndiyo walijitokeza,”alisema.
Mkufunzi kutoka NIT, Charles Kisunga, ni bora mafanikio yakaonekana ikizingatiwa watu hao wamekuwa ndiyo chanzo kikuu cha ajali barabarani.
Alisema mafunzo hayo ni maombi kutokaSerikalini na hadi sasa yametolewa Mtwara kwa washiriki 600, Lindi na Sengerema mkoani Mwanza.
Naye Mbunge wa Jimbo la Kahama, James Lembeli, ambaye ndiye mfadhili mkuu wa mafunzo hayo, alisema lengo kuu ni kuhakikisha bodaboda wanaepukana na ajali kwa kufuata sheria za usalama barabaarani kwa usahihi.
Post a Comment