Featured

Loading...


Kingunge Amtolea Uvivu Nape Nnauye......Ashauri Avuliwe Uongozi, Ashangaa Viongozi Kumfumbia Macho


Mwanasiasa mkongwe wa CCM, Kingunge Ngombale-Mwiru amemshukia Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye kwa kauli zake alizodai zinaminya demokrasia na kwamba CCM haiwezi kusimama wanapopambana wenyewe kwa wenyewe. 
 
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Kingunge (pichani), ambaye hivi karibuni aliweka bayana kumuunga mkono Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa katika harakati zake za kuwania urais, alisema hakubaliani na kauli ya Nape kuwa wagombea wasioridhika na uamuzi wa Kamati Kuu (CC), hawawezi kukata rufaa kwa sababu ya muda kuwa mfupi.
 
Alisema CCM imeweka utaratibu wa wanachama kudai haki zao ndani ya chama, pindi wasiporidhishwa na uamuzi wa vikao vya chini.
 
Alisema mwaka 2005, mgombea wa nafasi ya urais, John Malecela alikata rufaa katika Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) baada ya jina lake kutopelekwa.
 
“Aliyekuwa mwenyekiti wa chama wakati ule Mkapa (Benjamin), alikubali baada ya kushauriana na wenzake kwa sababu haikuwa zawadi, bali ni haki yake,” alisema.
 
Hata hivyo, alisema baada ya kujielezea mbele ya NEC na wajumbe kuulizwa, walikubali kuwa majina matano yaliyoletwa na CC yanatosha.
 
“Kufikiria kwamba mtu akose haki kwa sababu ya kukosa muda huko ni kuwakosesha watu haki,” alisema.
 
Kingunge alisema amani na utulivu ni mambo yanayojengwa kwa haki na lazima imani ijengwe na viongozi.
 
Alisema lugha za kibabe ambazo zimekuwa zikitolewa na baadhi ya viongozi huku chama kikaa kimya ndizo zinazowatia watu shaka.
 
“Sasa hivi kumekuwa na nguvu kubwa ya kupambana ndani ya chama kuliko wapinzani… nyumba ikigawanyika haiwezi kusimama na CCM haiwezi kusimama inapopambana yenyewe kwa yenyewe,” alisema.
 
Alisema kukiwa kuna jitihada za kunyima haki watu, kunaweza kusababisha machafuko.
 
“Asitokee mtu akadhani kuwa nchi ni yake pekee yake, sitaki kusema kwa sababu matokeo yake mnayajua. CCM ni yetu sote hata sisi tuliokuwapo tangu zamani,” alisema.
  
 “Ukisema wagombea hawataweza kukata rufaa unapotosha misingi, kwa nini unataka kuminya haki hiyo sasa? Ingekuwa wakati wetu na Mwalimu (Julius Nyerere), mtu wa namna hiyo tungemvua uongozi.”

Hata hivyo, Nape alipoulizwa alisema hawezi kujibu tuhuma hizo kwa kuwa hajamsikia na anayetakiwa kuzijibu ni aliyempa kazi.
 
“Siwezi kujibu kwa sababu sijamsikia, sijui kasema wapi, amesema nini na kama amesema mimi siwezi kujibu mwenye wajibu huo ni aliyenipa kazi,” alisema Nape.

TOA MAONI YAKO HPO CHN1 KUHUSU HABARI HII

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright JICHO LETU
Back To Top