Featured

Loading...


CCM Wamtimua Mwandishi wa Mwananchi Kwenye Msafara Wao Baada Ya Kuripoti Tukio la Magufuli KUZOMEWA Jijini Mbeya


Mwandishi wa gazeti la Mwananchi, Peter Elias ameondolewa kwenye kikosi cha waandishi wa habari wanaoandika habari za kampeni za uchaguzi za mgombea wa CCM, Dk John Magufuli kwa madai kuwa aliandika habari isiyostahili.

Hii ni mara ya pili kwa CCM kumtimua mwandishi wa gazeti la hilo kutoka kwenye msafara wa mgombea wake wa urais. Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2010 wakati ilipomtimua Midraj Ibrahim kwa kuripoti tukio ambalo chama hicho kikongwe hakikupenda litangazwe kwenye vyombo vya habari.

CCM imesema imechukizwa na kitendo cha mwandishi huyo kuripoti habari ya tukio la wanachama wa Chadema kumnyooshea alama ya vidole viwili na kumzomea mgombea wa CCM wakati aliposimama Uyole, Mbeya. Alama ya vidole viwili ni nembo iliyo kwenye bendera ya Chadema.

Elias amesema kuwa juzi mkurugenzi wa mawasiliano wa CCM, Godfrey Chongolo ndiye aliyemweleza kwamba chama hicho kimesikitishwa na habari hiyo, akidai kuwa kulikuwa na habari nyingi zaidi zinazomhusu mgombea huyo wa urais.

Elias alisema alielezwa na Chongolo kuwa CCM imeshindwa kuvumilia habari  ya magufuli kuzomewa akisema haikustahili kupewa uzito.

Mkurugenzi huyo alimwambia mwandishi huyo kuwa alitarajia kuona taarifa hiyo ikiripotiwa “Vijana wa Chadema wafanya fujo kwenye mkutano wa kampeni wa Dk Magufuli.”

Kutokana na habari hiyo, Chongolo alimtaka Elias kutoendelea kubaki katika kikosi cha waandishi kwa sababu anawaharibia katika vita wanayopigana kuelekea uchaguzi mkuu ujao.

“Unajua sisi tuko vitani, kwa hiyo unapoandika kwamba Wanachadema walimzomea kwa kuonyesha vidole viwili juu, maana yake ni kwamba hawamkubali mgombea wetu, sasa hapo unawaeleza nini Watanzania?”

“Siku ile ya tukio Magufuli alifanya mikutano ya barabarani zaidi ya mitano, nashangaa ninyi mkaona ile ndiyo habari ya kuandika na kuacha nyingine za maana,” alisema Elias akimnukuu Chongolo.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alipoulizwa kuhusu suala hilo alisema amesikia na baadaye akakata simu.

Akizungumzia uamuzi huo Mhariri Mtendaji Mkuu wa MCL, Bakari Machumu alisema kampuni imesikitishwa na hatua hiyo lakini haitakatishwa tamaa katika kutekeleza majukumu yake kwa umma.

TOA MAONI YAKO HPO CHN1 KUHUSU HABARI HII

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright JICHO LETU
Back To Top