Jay Z na Beyonce

...Wakiwa na mtoto wao Blue Ivy
Diamond Platnumz na mpenzi wake Zarinah Hassan 'Zari the Boss Lady' wakiwa na mtoto wao, Latiffah Nasbul 'Tiffah'.

Mastaa na shoo za ‘kiprofesheno’ SEAN
Carter ‘Jay-Z’ ni jina kubwa sana duniani kufuatia mchango wa msanii
huyo katika gemu la muziki wa Hip Hop. Kupitia umaarufu wa jina lake,
umeweza kumpatia mafanikio makubwa na hata kumsaidia mwanaye, Blue Ivy
Carter kuvunja rekodi akiwa bado tumboni kwa mamaye siku chache tu baada
ya kuzaliwa.
Jambo hilo lililotokea kwa Jay-Z ndilo
limetokea pia kwa msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
pamoja na mwanaye Tiffah. Katika makala haya yanachambua baadhi ya vitu
vinavyoshabiiana kati ya mastaa hao;
Jay-Z na Blue Ivy Historia ya msanii
huyu imekuwa ikiwavutia wengi kutokana na jinsi alivyoanza kazi yake ya
muziki akiuza CD mkononi kutokana na kukosa msimamizi mpaka mwaka 1996
alipoachia albamu yake ya kwanza iitwayo Reasonable Dought iliyofanya
vizuri.
Kwa upande wa ujasiriamali na uwekezaji,
anamiliki Klabu 40/40, ni mhisani katika kampuni ya nguo za Rocawear,
mdau katika Studio ya Roc- A-Fella na mmiliki wa Kampuni ya Roc Nation.
Kwa upande wa mwanaye, Blue Ivy
aliyemzaa na mwanamuziki wa R&B, Beyonce Knowles alianza kuvunja
rekodi kabla hata hajazaliwa baada ya mamaye kutangaza kuwa ana ujauzito
kwenye Tamasha la Ugawaji Tuzo za MTV mwaka 2011 ambapo ndani ya
sekunde moja zaidi ya watu 8,868 walishare taarifa hiyo.
Blue Ivy alivunja rekodi nyingine baada
ya kuzaliwa kwa kutajwa kuwa mwanamuziki mdogo kuwahi kutokea kwenye
Chati za Billboard kwa kushirikishwa kwenye wimbo wa baba yake uitwao
Glory. Mbali na rekodi hizo mtoto huyo mwenye miaka mitatu kwa sasa
amepata dili kwenye makampuni mengi ya mavazi, ameshirikishwa kwenye
nyimbo kadhaa za wazazi wake na inasemekana ndiye motto maarufu zaidi
duniani. Diamond Platnumz na Tiffah Diamond pia ana historia ya kuvutia
ambapo mwaka 2009 alitoa Wimbo wa Nenda Kamwambie kasha mwaka 2010
kuvunja rekodi ya kuwa msanii wa kwanza Tanzania kuchukua tuzo tatu za
Kili Music.
Diamond amewahi pia kuvunja rekodi kwa
kuwa msanii wa kwanza kuuza zaidi ya kopi 1200,000 za albamu na msanii
wa kwanza kufanya shoo iliyoitwa Diamond are Forever na kuuza zaidi ya
tiketi 1,500 kwa kiingilio cha Sh. 50,000.
Mbali na tuzo nyingi alizochukua, Diamond amewahi kuwa balozi wa makampuni mengi nchini ikiwemo Coca Cola.
Kwa upande wa bintiye Tiffah, mbali na
kupata umaarufu tu akiwa tumboni mwa mama yake Zarinah Hassan, alianza
kuvunja rekodi ya kwanza kwa kupata zaidi ya
wafuasi 2,000 kwenye ukurasa wake wa
Instagram chini ya saa 24 tangu kuzaliwa kwake. Lakini pia hadi anafanya
sherehe ya kutimiza siku 40, tayari kwenye ukurasa huo alikuwa na
wafuasi 126,000 ambao umemfanya kuwazidi baadhi ya mastaa nchini.
Mbali na kuvunja rekodi hizo ambazo
hazijawahi kuwekwa na mtoto yeyote yule wa staa Bongo,Tiffah pia ni
balozi wa Pugu Mall na Msasani City Mall kwa upande wa maduka ya nguo za
watoto ambapo anavishwa bure kwa mwaka mzima.
Post a Comment