Featured

Loading...


Mgombea ubunge ‘atoweka’, wazazi watumiwa ujumbe wa vitisho

Mgombea ubunge wa Chama cha ACT-Wazalendo katika Jimbo la Bariadi Magharibi, Masunga Nghezo. Picha na Mpigapicha wa ACT-Wazalendo.

Mbali na kutoonekana kwa Nghezo, simu yake aliyokuwa akiitumia, ndiyo inatumika kutuma ujumbe wa vitisho kwenda kwa mzazi wa mgombea huyo ikimtaka amkanye mwanae kuachana na siasa vinginevyo familia nzima itadhurika. By Emmanuel Mtengwa, Mwananchi Digital

Bariadi. Mgombea ubunge wa Chama cha ACT-Wazalendo katika Jimbo la Bariadi Magharibi, Masunga Nghezo ametoweka kusikojulikana na hajapatikana hadi sasa akiwa katika harakati za kufanya mikutano ya hadhara katika jimbo hilo.

Mbali na kutoonekana kwa Nghezo, simu yake aliyokuwa akiitumia, ndiyo inatumika kutuma ujumbe wa vitisho kwenda kwa mzazi wa mgombea huyo ikimtaka amkanye mwanae kuachana na siasa vinginevyo familia nzima itadhurika.

Taarifa ya chama hicho iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari na Afisa Habari wake, Abdallah Khamis, imesema kuwa Nghezo alitoweka siku ya Jumatatu ya wiki hii akijiandaa kwenda katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha Baneni.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa kabla ya kutoweka kwake, Nghezo, alienda kumtafuta dereva mwingine wa kumuendesha baada ya yule wa siku zote kwenda msibani na kwamba aliporudi na dereva mwingine aliliacha gari likiwa katika maandalizi ya kufungwa vipaza sauti.

Taarifa imeongeza kuwa baada ya dereva na viongozi wengine wa chama kumaliza kazi ya kufunga vipaza sauti walianza kumtafuta mgombea wao bila mafanikio huku simu yake ikiwa haipatikani hadi jana mzee wake alipopokea ujumbe mfupi wa simu kupitia simu ya mwanae ikimtaka kumkanya mwanae aachane na siasa za Bariadi.

Pia taarifa ya Khamis inaeleza kuwa mzazi wa mgombea, Mzee Nghezo, anazidi kutumiwa ujumbe wenye masharti wakimpa muda wa saa sita kutekeleza masharti yao vinginevyo watamdhuru kijana wake na kisha kuitafuta familia nzima,

Hata hivyo Mwananchi Digital imezungumza na mzazi wa mgombea huyo, Joseph Nghezo ambaye amethibitisha kupotea kwa mtoto wake tangu siku ya Jumatatu.

Mzee Nghezo amesema kuwa siku ya Jumatatu viongozi wa chama cha ACT-Wazalendo walimpigia simu wakitaka kujua kama mtoto wake yupo nyumbani, ndipo alishtuka kwakuwa alijua mwanawe yuko kwenye kampeni.

Ameongeza kuwa baada ya kuulizwa sana juu ya mtoto wake, majirani walimshauri aende akatoe taarifa katika kituo cha polisi.

‘’Tumeenda kutoa taarifa katika kituo cha polisi hapa mjini Bariadi na polisi wamechukua maelezo hivyo wanafanya kazi’’ aliongeza Nghezo.

Mwananchi Digital imemtafuta Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Simiyu, Gemini Mushi ili kuthibtisha tukio hilo lakini hakuweza kuzungumza lolote kwakuwa alipopokea simu alisema yuko kwenye kikao.

TOA MAONI YAKO HPO CHN1 KUHUSU HABARI HII

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright JICHO LETU
Back To Top