Uchambuzi wa magazeti @CloudsFM
umekupita? kazi yangu ni kuhakikisha zile zote kubwa za leo hazikupiti,
kama hukuweza kuzisikia zote, karibu ucheki na hizi nyingine hapa
chini.
Magufuli apaa utafiti wa Urais, utafiti wa TWAWEZA wazua mjadala na maswali mengi kwa raia, wasomi na waharakati, Mgombea Urais kupitia Chama cha UPDP Fahmi Dovutwa amewataka wananchi kuchagua sera zitakazowafaa na kuzichuja bila kufuata ushabiki.
Mgombea Urais kupitia CHADEMA Edward Lowassa asema jibu halali la utafiti wa TWAWEZA litapatikana October 25, Wasomi wengi wanaujadili utafiti wa TWAWEZA wasema matokeo halisi ya utafiti huo yatapatikana siku ya Uchaguzi Mkuu October 25 ikiwa ndio siku pekee kujua ukweli wa majibu ya utafiti huo.
Wadau wengi ikiwemo Maprofesa wa vyuo mbalimbali wamejitokeza kupinga utafiti wa TWAWEZA
wakisema utafiti huo hauendani na hali halisi ya kisiasa nchini, wasema
matokeo hayo hayawezi kutabiri ushindi kati ya Mgombea urais wa CCM Dk. John Magufuli na Mgombea urais wa CHADEMA Edward Lowassa.
Mgombea Urais kupitia CCM Dk. John Magufuli
atoa style mpya ya kuomba kura kwa kuanza na kupiga push-up kabla ya
kumwaga sera zake na walemavu wa kusikia wamevitaka vyama vya Siasa
kuweka wakalimani wa lugha za alama kwenye kampeni za Madiwani, Wabunge na Rais.
Uchambuzi wote wa magazeti kwenye #PowerBreakfast nimeurekodi na kukuwekea sauti yake hapa chini, bonyeza play kusikiliza.
Post a Comment