Featured

Loading...


Hatimaye Wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Dodoma Waruhusiwa Kupiga Kura


MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Gallawa amesema wanafunzi wa vyuo vikuu waliojiandikisha Dodoma watapiga kura kwenye maeneo waliyojiandikisha.
 
Alisema hayo jana wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya uchaguzi mkuu utakaofanyika kesho.
 
Baadhi ya vyuo vya mkoa huo ni Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Chuo Kikuu cha St. John, Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Chuo cha Serikali za Mitaa, Chuo cha Mipango na Chuo cha Madini.
 
Akijibu moja ya maswali ya waandishi wa habari ni wapi wanafunzi wa vyuo vikuu watapiga kura kutokana na utata uliopo kuwa si wakazi wa mkoa wa Dodoma na kwamba kuna taarifa kuwa watasafirishwa kwa mabasi ili kufika Dodoma kupiga kura.
 
Gallawa alisema tume ilitaka watu wajiandikishe kituo chochote lakini kuna baadhi ya vituo viliandikisha watu wengi wa nje kuliko wakazi wa eneo husika, hali inayozua maswali mengi kuwa wakazi wa pale watachaguliwa diwani.
 
“Mfano utakuta kata ina watu 1,700 ambao si wakazi waliojiandikisha, wanafikia 5,000 lakini ukiangalia kwa undani suala hili utaona hali halisi ilivyo,” alisema.
 
Katika hatua nyingine, wasimamizi wa uchaguzi kwenye wilaya zote saba za mkoa wa Dodoma wameshapokea fedha za kuendesha uchaguzi mkuu na mafunzo kwa watendaji watakaoshiriki katika uchaguzi yanahitimishwa kwenye wilaya zote.
 
Waliojiandikisha ni wananchi 1,053,136 kuwa wapiga kura sawa na asilimia 102.7 ya lengo, ambapo lengo lilikuwa ni kuandikisha wapigakura 1,025,084.

TOA MAONI YAKO HPO CHN1 KUHUSU HABARI HII

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright JICHO LETU
Back To Top