Featured

Loading...


MAGUFULI AKUBALI MDAHALO, LOWASA AKATAA KUSHIRIKI

  
Kitendo cha Lowassa kutokuwapo katika mdahalo huo utakaofanyika kesho saa 7:30 mchana hadi saa 10 jioni, kutapunguza ushindani miongoni mwa wagombea wakuu wawili ambao wanachuana vikali katika uchaguzi unaotajwa kuwa wa kihistoria.
Dar es Salaam. Siku moja kabla ya kufanyika kwa mdahalo wa wagombea urais nchini, Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) umesema mgombea wao kupitia Chadema, Edward Lowassa hatashiriki shughuli hiyo huku CCM ikithibitisha mgombea wake, Dk John Magufuli kushiriki.
Kitendo cha Lowassa kutokuwapo katika mdahalo huo utakaofanyika kesho saa 7:30 mchana hadi saa 10 jioni, kutapunguza ushindani miongoni mwa wagombea wakuu wawili ambao wanachuana vikali katika uchaguzi unaotajwa kuwa wa kihistoria.
Licha ya vyama vinane kusimamisha wagombea urais, vinavyochuana zaidi ni Chadema chini ya mwamvuli wa Ukawa na CCM, huku ACT-Wazalendo ikionekana kuleta upinzani.
Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu aliliambia Mwananchi jana kuwa, kwa sasa mgombea wao yupo katika Kanda ya Ziwa kwenye kampeni, hivyo itakuwa ngumu kuhudhuria mdahalo huo unaosubiriwa kwa hamu.
Hata hivyo, wakati Lowassa akikosekana katika mdahalo huo, Mkurugenzi wa Taasisi ya Twaweza, Aidan Eyakuze alisema hadi jana vyama vinne vilikuwa vimethibitisha ikiwamo CCM.
Vyama vingine vitakavyoshiriki mdahalo huo kwa mujibu wa Eyakuze ni Alliance for Democratic Change (ADC), ACT-Wazalendo na Chaumma.
Alisema jana walipokea barua ya uthibitisho kutoka CCM ikisema itashiriki, hivyo kuongeza idadi ya vyama vitakavyochuana hadi kufikia vinne kati ya vitano ambavyo vilikidhi vigezo vya kushiriki mdahalo.
“Tunatarajia atakuwapo Dk John Magufuli katika mdahalo wetu na bado tunaendelea na mazungumzo na Ukawa ili watupatie majibu kwa maandishi kama watashiriki au la.
“Mlango wetu utakuwa wazi kuhakikisha tunawapatia fursa ya kujibu maswali ya wananchi watakayowauliza, lakini tumeshaeleza kuwa watakaoshiriki mdahalo huu ni wagombea wa urais na siyo vinginevyo,” alisema Eyakuze.
Hata hivyo, Mwalimu alisema suala la muda ni kikwazo kwao kitakachofanya mgombea wao kutoshiriki mdahalo huo ulioandaliwa na Twaweza, Tanzania Media Foundation (TMF), Taasisi ya CEO roundtable na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa).
“Huwezi kumwondoa mgombea kwenye kampeni aende kwenye mdahalo akatumie siku mbili kujiandaa na kusafiri bila kuwafikia wananchi vijijini ambao wanamsubiri kwa hamu, kifupi sisi tunawatakia kila la kheri,” alisema Mwalimu kwa njia ya simu.
Naye Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi, Uendeshaji na Utawala wa ADC, Jumanne Magafu alipendekeza maboresho ya sheria ya uchaguzi ili midahalo iwe sehemu ya mchakato wa Uchaguzi Mkuu siku zijazo.
Alisema kwa sasa hakuna sheria wala kanuni zinazowalazimisha watu muhimu kama wagombea wa urais kuhudhuria midahalo na kujibu maswali ya wananchi, jambo ambalo huwa ni adimu katika mikutano yao ya kampeni.
“Tunaendelea kujiandaa vizuri na mdahalo huu, mgombea wetu wa urais, Anna Mghwira kwa sasa yupo kwenye kampeni atarudi kesho maalumu kwa ajili ya shughuli hiyo ya Jumapili,” alisema Vanance Msebo, Mkurugenzi wa Kampeni wa ACT-Wazalendo

TOA MAONI YAKO HPO CHN1 KUHUSU HABARI HII

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright JICHO LETU
Back To Top