Featured

Loading...


Update Kuhusu Helikopta ya CCM Iliyoanguka Mbugani Ikiwa na Mbunge Deo Filikunjombe


Usiku wa kuamkia leo October 16 2015 majukwaa  ya siasa Tanzania yametawaliwa na ajali ya Helikopta ambayo imeanguka na kulipuka kwenye mbuga ya Wanyama ya Selous ambapo Waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyalandu alithibitisha kwamba mmoja wa waliokuwemo ndani ni Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe (CCM).

Kupitia  ukurasa  wake  wa  Twitter,Nyalandu  aliandika;
"Tumetuma vikosi vya maafisa na maaskari katika eneo la Selous kulikotokea ajali ya helikopta katika harakati za uokozi, ajali ya helikopta imetokea katika kitalu R3 ndani ya mbuga ya Selous na mashuhuda wanasema ilianguka na kulipuka ng’ambo ya mto Ruaha

"Mashuhuda wa ajali ya helikopta iliyotokea Selous walikuwa kitalu R2 na walishuhudia ikianguka na kulipuka ng’ambo ya mto Ruaha Kitalu R3, Maafisa na Maaskari wanaelekea eneo la tukio kutokea Msolwa na Matambwe na tumeagiza vikosi vilivyo kwenye doria Selous kushiriki uokoaji

"Mashuhuda wa ajali ya helikopta Selous walikuwa Kitalu R2 wanasema ilianguka baada ya majira ya saa 12 jioni na kulipuka, serikali kupitia wizara ya maliasili na utalii inachukua hatua zote kuwafikia wahanga na majeruhi wa ajali ya helikopta Selous usiku huu

"Nimeagiza section 2 zenye askari 16 kutoka Matambwe na Msolwa (Selous) kwenda eneo la tukio, RPC Morogoro na mkuu kanda ya Msolwa (Selous) wanashirikiana, hatujui kitakachokuwa kimewapata wasafiri ndani ya helikopta iliyoanguka akiwepo Mh, Filikunjombe, tuungane kuwaombea kwa Mungu"

Katika taarifa nyingine kutoka upande wa CCM iliyotolewa na naibu waziri wa mawasiliano sayansi na teknolojia January Makamba mida ya saa sita usiku ilisema "Tumesikia habari za chopa kuanguka huko Selous. Mungu aepushe kusiwe na majeruhi. Chopa zote zinazotumiwa na CCM kwenye kampeni ziko salama"

Baadae aliandika :"Kwakuwa ilisemekana kuwa chopa ya kampeni ya CCM imeanguka, tulifuatilia/kubaini/kuripoti kuwa tulizokodi kama Chama hakuna iliyoanguka". Hiyo ndio ilikua tweet ya mwisho kuandikwa na January Makamba usiku lakini badae aliretweet kilichoandikwa na Waziri Nyalandu na Zitto Kabwe.

Zitto aliandika: "Naomba utulivu.(1) ajali ya helkopta imethibitishwa (2) kuwaka hakujathibitishwa (3) ndugu yangu Deo alikuwamo (4) hakuna uthibitisho wa madhara, naomba utulivu mpaka tupate taarifa rasmi zilizothibitishwa na mamlaka husika, naomba sana hilo ili kuepuka sintofahamu"

TOA MAONI YAKO HPO CHN1 KUHUSU HABARI HII

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright JICHO LETU
Back To Top