Featured

Loading...


Jengo la ghorofa mbili labomoka na kuua watu 17 Uchina

Jengo la ghorofa mbili limebomoka katika mkoa wa Henan, katikati mwa Uchina na kuua wafanyakazi mjengo 17 na kujeruhi wengine 23, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti.

Maafisa wa uokoaji wamekuwa wakifanya kazi usiku kucha kuondoa miili ya waliofariki pamoja na kutoa majeruhi kutoka kwenye vifusi. Mkasa huo umetokea katika eneo la Beiwudu, wilaya ya Wuyang.

Tisa kati ya waliojeruhiwa wanatibiwa katika hospitali iliyoko mji wa Luohe, na wamo katika hali mahututi, maafisa wamesema. Maafisa hao wamesema wafanyakazi hao wa mjengo walikuwa wakifanyia ukarabati msingi wa jumba hilo ajali hiyo ilipotokea.

Serikali ya wilaya ya Wuyang sasa imesitisha juhudi za uokoaji. Uchunguzi umeanza kuhusu nini hasa kilichosababisha mkasa huo ambao umeibua tena wasiwasi kuhusu kutekelezwa kwa kanuni za usalama kuhusu majengo nchini Uchina.

Mwezi Mei, jumba la kutunza wazee liliteketea mkoani Henan na kuua watu 38. Ilibainika baadaye kwamba jumba hilo lilijengwa vibaya kwa kutumia vitu vinavyoshika moto haraka.

Mmoja wa manusura aliambia kituo cha runinga cha serikali cha CCTV kwamba wafanyakazi hao walitoka mji wa Nanyang kusini-magharibi mwa mkoa wa Henan.
Jengo hilo lilijengwa miaka ya 1990.

TOA MAONI YAKO HPO CHN1 KUHUSU HABARI HII

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright JICHO LETU
Back To Top