WAGENI wa kimataifa zaidi ya 50 wanatarajiwa kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Tanzania, Dk John Magufuli zitakazofanyika keshokutwa jijini Dar es Salaam.
Ofisa
Uhusiano wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Rosemary Malale, alisema orodha hiyo ya wageni walioalikwa, inajumuisha
mashirika ya kimataifa, mashirika ya kikanda, wakuu nchi na mabalozi.
Rais
mteule Dk Magufuli alitangazwa kuwa mshindi, baada ya kushinda katika
uchaguzi, uliofanyika wiki iliyopita kwa kupata asilimia 58.46 ya kura
zote zilizopigwa. Ofisa huyo alisema wizara pia imetuma mialiko kwa nchi
za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), inayoundwa na Kenya, Uganda,
Rwanda na Burundi.
Nchi
nyingine zilizoalikwa ni za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa
Afrika (SADC), Umoja wa Ulaya (EU) na Umoja wa Afrika (AU).
Aidha,
sherehe hizo pia zinatarajiwa kuhudhuriwa na Muungano wa nchi za
Amerika (ISSR), Misri, Ghana, Sweden, Uingereza, Marekani, Ufaransa,
Japan, China na Umoja wa Mataifa.
Maandalizi
ya sherehe hizo zitakazofanyika katika uwanja wa Uhuru, jijini Dar es
Salaam yanaendelea, yakihusisha wanajeshi ambao pamoja na mazoezi
mbalimbali, pia zilionekana ndege za kivita angani.
Dk
Magufuli aliwaangusha wagombea wengine saba, akiwemo mpinzani wake mkuu
kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupitia Umoja wa
Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa.
Wakati
rais huyo mteule akisubiri kuapishwa, kumekuwa na ushauri tofauti
kutoka kwa watu wa kada mbalimbali, wakitaka atekeleze ahadi zake na pia
kujenga umoja wa Watanzania.
Akizungumza
jana na mwandishi wa habari hizi, mmoja wa waliogombea urais, MacMillan
Lyimo (TLP), alisema alimtaka Magufuli akiingia madarakani, ahakikishe
anajenga umoja miongoni mwa Watanzania kwa kuepuka kujenga chama chake
pekee.
Post a Comment