Featured

Loading...


MABULA: "SIKUJA KUITENGUA TORATI


 Na:George Binagi-GB Pazzo & Vesterjtz.

Mbunge Mteule wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Stanslaus Shing’oma Mabula, amewahakikishia Machinga Jijini Mwanza kuwa wataendelea kufanya biashara zao katika maeneo mbalimbali ya katikati ya Jiji hilo kama yaliyotengwa na uongozi wa halmashauri.


Mabula aliyasema hayo jana wakati akiwashukuru wakazi wa Jimbo hilo kwa kumchagua kuwa mbunge wao katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Mbugani, kufuatia uvumi unaoezwa mitaani kwamba machinga pamoja na mamantilie wataondolewa katikati ya Jiji la Mwanza kufuatia ushindi wake.


“Mtu kaenda Makoroboi, Stand ya Tanganyika, Sahara, Soko la Igoma pamoja na maeneo mengine na kuwaambia Machinga na Mamantilie kuwa Mabula ameingia madarakani, cha moto mtakiona. Nataka msikilize kauli yangu leo kwamba sikuja kulitengua torati, nitaendelea kushirikiana na ninyi ili muwe bora, tena zaidi ya miaka mitano iliyopita”. Alisema Mabula.


Katika hatua nyingine Mabula amewashukuru wakazi wa Jimbo la Nyamagana kwa kumuamini na kumchagua kuwa mbunge wao, kwani wakati akiwa Mstahiki wa Jiji la Mwanza yeye pamoja na wanaccm wenzake walisemewa mambo mengi mabaya ambayo kimsingi hayakuwa na ukweli wowote.


“Wamama walinyanyasika sana, walitemewa mate, walichaniwa nguo, walipondwa mawe, walitukanwa, walidharirishwa. Pia tulisemewa na kushuhudiwa uongo kila kona. Ninyi wenyewe mnakumbuka tuliambiwa tumevunja matorori, tumeiba maandazi , lakini nawashukuru maana wananchi wa Nyamagana walisema huyo huyo alieiba maandazi, kumwaga mchele na kuvunja matorori ndie atakuwa mtetezi wetu.


Nae Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtatu, aliwashukuru Watanzania wote kwa kukichagua chama hicho kuanzia ngazi ya Madiwani, Wabunge pamoja na Rais ambapo Dkt.John Pombe Magufuli aliibuka na ushindi wa asilimia 58.46

Katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Jumapili iliyopita ya Octoba 25 kote nchini, Mabula aliibuka mshindi katika Jimbo la Nyamagana kwa kupata kura 81,017 na hivyo kumuondoa aliekuwa mbunge wa jimbo hilo Ezekiel Wenje kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema aliepata Kura 79,280.

TOA MAONI YAKO HPO CHN1 KUHUSU HABARI HII

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright JICHO LETU
Back To Top