Featured

Loading...


Wanasheria wapinga urais wa Dk. Shein

Wakati uamuzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec) kufuta matokeo ya uchaguzi visiwani humo ukiendelea kuibua mijadala, Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) kimeibuka na kupinga uhalali wa kubaki madarakani kwa Rais wa sasa visiwani humo, Dk. Ali Mohamed Shein.

Msimamo huo wa kupinga uhalali wa Dk. Shein kubaki madarakani lilitolewa na Rais wa ZLS, Awadh Ali Said, lengo likiwa ni kutoa mtazamo wao kisheria kuhusiana na kile kilichoelezwa juzi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud Mohamed, aliyedai kuwa Dk. Shein ataendelea kuwapo madarakani hadi hapo uchaguzi wa marudio utakapofanyika na mshindi kutangazwa. Hata hivyo, Awadh hakueleza kama ni msimamo wa ZLS au wa kwake binafsi.

Akieleza zaidi, Rais huyo wa ZLS alisema kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Dk. Shein amefikia ukomo wa uongozi wake jana (Novemba 2) na kwamba, hivi sasa hana tena uhalali wa kisheria wa kuwapo madarakani.

Awadh, alisema kwa mujibu wa kifungu cha 28 (2) cha katiba hiyo ya Zanzibar, ukomo wa rais wa kukaa madarakani ni miaka mitano tangu alipoapishwa na muda huo ulimalizika Novemba 2 mwaka huu (jana).

Aliongeza kuwa kifungu cha 28 (1) cha Katiba ya Zanzibar, kimeeleza wazi kuwa rais ataendelea kuwa na wadhifa wake hadi rais anayefuata atakapokula kiapo cha kuwa rais katika mazingira maalum kama kufanyika kwa uchaguzi mdogo iwapo rais atalivunja Baraza la Wawakilishi kwa kupoteza imani nalo na kuitisha uchaguzi, au wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kupoteza imani na Rais na kulazimika kuvunjwa Baraza hilo na kuitisha uchaguzi mdogo na siyo kwa mazingira ya sasa.

Alisema kuwa hivi sasa, Serikali kukitumia kifungu cha 28 (1) kuhalalisha kuwapo madarakani kwa Dk. Shein ni uvunjwaji wa katiba, kifungu cha 28 (2) kinachozungumzia ukomo wa muda wa urais kubakia madarakani tangu kuapishwa kwake.

 “Kifungu walichokitumia kinaweza kuwa na nafasi ya kuruhusu rais kubakia madarakani kama Baraza la Wawakilishi limemshitaki na kupoteza imani naye na kuamua kulivunja na kuitisha uchaguzi mdogo… hapo anaweza kubakia na wadhifa wake hadi uchaguzi utakapofanyika na kuapishwa rais mpya,” alisema Awadh, ambaye ni wakili wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.
-Nipashe

TOA MAONI YAKO HPO CHN1 KUHUSU HABARI HII

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright JICHO LETU
Back To Top