
Kocha mpya wa Chelsea, Guus Hiddink.
Aliyekuwa Kocha wa Timu ya Taifa ya Uholanzi, Guus Hiddink ameteuliwa kuwa kaimu meneja wa Chelsea hadi mwisho wa msimu huu.
Hiddink ameteuliwa baada ya Jose Mourinho kutimuliwa Alhamisi iliyopita.
“Nimefurahia kurejea Stamford Bridge. Chelsea ni moja ya klabu kubwa
duniani lakini haipo pale inakofaa kuwa kwa sasa. Hata hivyo nina
uhakika tunaweza kubadilisha mambo,” amesema Hiddink baada ya kuteuliwa.
“Nasubiri kwa hamu kufanya kazi na wachezaji na wakufunzi wenzangu
wapya katika klabu hii kubwa na kufufua uhusiano wangu mzuri na
mashabiki wa Chelsea.”
Mholanzi huyo alikuwa uwanjani Stamford Bridge kutazama mechi ya Ligi
Kuu England dhidi ya Sunderland ambayo ilisimamiwa na Steve Holland
akisaidiwa na Eddie Newton, ambaye sasa atakuwa kocha msaidizi wa timu
hiyo.
Hiddink, aliwahi kuinoa Chelsea wakati mmoja, alipowasaidia kushinda Kombe la FA mwaka 2009, lakini bado hajatia saini mkataba.
Hiddink alishinda mataji sita ya Ligi ya Uholanzi na Kombe la Ulaya
akiwa meneja wa PSV Eindhoven ya Uholanzi katika vipindi viwili.
Pia aliongoza Timu za Taifa za Korea Kusini, Australia na Urusi kabla
ya kujiunga na Chelsea mara ya kwanza kujaza pengo lililoachwa na Luiz
Felipe Scolari Februari 2009.
Alijiuzulu wadhifa wake kama mkufunzi wa timu ya Taifa ya Uholanzi
mwezi Juni, baada ya kutofanya vyema katika juhudi za kuwasaidia kufuzu
kwa Euro 2016.
TOA MAONI YAKO HPO CHN1 KUHUSU HABARI HII
KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK
During its two year run, the project will award approximately 100 major
reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for
stories on development issues.
Journalists who produce the best stories published or broadcasted in
media that reach African audiences, will win a major international
reporting trip.
During its two year run, the project will award approximately 100 major
reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for
stories on development issues. Journalists who produce the best stories
published or broadcasted in media that reach African audiences, will win
a major international reporting trip.
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;
Filed Under:
MICHEZO
on Sunday, 20 December 2015
Post a Comment