
Kama umeshakuwa kwenye mahusiano ambayo hayakudumu au umekuwa na
changamoto kwenye kumtafuta mpenzi ambaye utadumu naye kwa muda mrefu,
Wazo lakuwa na mahusiano yenye furaha na yakudumu kwamuda mrefu
linaonekana kama haliwezekani. Kwauhakika kuna hatua za kuchukua ili
kuongeza thamani na muda wa mahusiano yeko.
Kama utaingia kwenye mahusiano ambayo hayatawalinda na kuwakinga afya zenu, wewe na mpenzi wako mtakuwa na mahusiano magumu sana ulimwenguni nayasiyo na furaha.
ANZISHA MAHUSIANO SAHIHI.
Elewa unataka nini na unahitaji nini.
Kuelewa hisia zako zinataka nini na mwili wako unahitaji nini kwenye mahusiano nimuhimu kabla yakuingia kwenye mahusiano kwakuwa unahitajika kufahamu hayo ili kufanikiwa kwenye mahusiano. Inawezekana tayari ushajua unataka nini na unahitaji nini kwenye mahusiano, Lakini hauna uhakika, Unaweza kujiuliza haya maswali.- Fikiria kwenye mahusiano yaliyopita nikitugani kilifanikiwa na kitu kipi hakikufanikiwa. Uzoefu huo unakwambia nini?
- Fikiri jinsigani ulikuwa guswa na watu pamoja na matukio. Kwamfano ilikuwa nivigumu kumuamini mtu au ilikuwa vigumu kuelezea hisia zako?
Itakusaidia wewe kuyatambua haya binfsi kabla ya kuingia kwenye mahusiano serious.
Hakikisha unakuwa kwenye mahusiano yatakayo kulinda afya yako kuliko kukupotezea uhai wako.- Sababu ya kiafya kuwa kwenye mahusiano: Kuhakikisha mna share love pamoja na kupeana kampani; kukuwa pamoja; kusaidiana kihisia na hata kimwili pale unapodhoofika kwakila mmoja nakutengeneza familia ya pamoja. Nimuhimu kutambua kuwa hisia sio kufanya ngono na kusaidian, bali kutoa kwa manufaa yako.
- Kuathiri kiafya nikama: Kuwa kwenye mahusiano kwahofu yakuwa mwenyewe, kuogopa kuachwa, na kuogopa kutengwa na familia, ndugu, jamaa na hata marafiki kwakuachana na mpenzi wako au kutokuwa na mtu flani. Kuwa makini kwakufanya ngono salama, kutoshawishika kwanjia ya fedha, usiwe kwenye mahusiano kama kulipiza kisasi kwa ex wako kwamaana sio sahihi kwa afya yako.
Kama utaingia kwenye mahusiano ambayo hayatawalinda na kuwakinga afya zenu, wewe na mpenzi wako mtakuwa na mahusiano magumu sana ulimwenguni nayasiyo na furaha.
Chagua mtu wakuwa naye kwahekima.
Kama unataka kuwa na furaha na mahusiano ya muda mrefu, Unatakiwa kuchaguwa mtu wakuwa naye kwaumakini sana. Wachunguzi wa mambo wanaamini kuwa wapenzi ambao wana share mawazo sawa, malengo sawa, wanashabikia vitu vinavyo endana kwujumla wamekuwa na mahusiano yenye mafanikio kuliko wengine.- Siolazima kwenye mahusiano muendane kilakitu, Lakini kama metofautiana kwaasilimia kubwa utaambulia maumivu.
Kuwa mkweli.
Kuingia kwenye mahusiano kunategemeka kutokuwa na ugumu au changamoto sio ukweli. Lakini kuonyesha hisia zako zaukweli nakuacha kuficha mambo kutakusaidia kuwa na mahusiano mazuri haswa kukiwa na ukweli kwenye kila jambo hadi hisia.Usijaribu kubadilisha malengo yako.
Wakati unaweza kupambana na maisha kwakufuata misimamo yako na malengo yako kwenye maisha, Lakini kwakufikiri unaweza kumbadilisha mtu, mitazamo au tabia yake hayo yatakupelekea kushindwa kwenye mahusiano. Hutakiwi kubadilisha mipango yako au yamtu mwingine mkiwa kwenye mahusiano.- Mawazo juu ya dini.
- Mawazo na mitazamo juu ya kuwa na watoto.
- Kubadilisha anayo yafanya wakati kakasirika.
- Kubadilisha mahusiano yampenzi wako na familia yake.
Usifikiri kuwa mnatakiwa kufanya kilakitu pamoja.
Wapenzi wengi wanaamini kuwa kufanya kila kitu kwapamoja ndiyo chachu
mojawapo yakuwaongezea mahusiano yao. Lakini kiukweli ndiyo chachu
yakuharibu mahusiano yenu. Usiache kujumuika pamoja na marafiki au
familia kwasababu y ampenzi wako na au kuendelea na hobbies yako kisa
kuwekeza kwenye mapenzi!
Usiharakishe mambo.
Watuwengi wanapoingia kwenye mahusiano wanapenda kuharahisha mambo
yafikie kwenye undani zaidi kama uchumba nakisha ndoa au kuishi pamoja.
Wakati unataka kufikia furaha yako hiyo inaweza ndiyo wakati unaipelekea
kuisha. Chukua muda kufikia kufahamiana na kupendana, Kwenye mahusiano
wengi tunaamini mwanzoni ndio tunapendana lakini kiukweli mwanzoni ndio
tunatamaniana natunapoanza kuzoeana ndipo tunapendana.
SIMAMIA MAHUSIANO YA FURAHA NA YAKUDUMU.
Tarajia mahusiano yako kubadilika.
Kama wewe na mawazoyako yanavyo badilika mahusiano yako nayo lazima
yabadilike nakukuwa. Kuliko kukaa nakutaka kufanya mahusiano yako yawe
sawa na yaliyo pita jitahidi na kupambana kuyabadilisha kujenga
mahusiano ya kudumu.Usiharakishe mambo.
Kubali kuwekeza muda, nguvu na juhudi kwenye mahusiano.
Kupata mahusiano ya furaha na yakudumu kunajumuisha muda, nguvu na
juhudi. Kinyume nakufikiri kuwa mahusiano ni 'Kazi ngumu', fikiri juu
yake kama maendeleo na tegemea kuwa na muunganiko pamoja na mpenzi wako
mki share pamoja. Japokuwa hili linawezekana likaonekana jambo gumu hapo
awali lakini kutakuwa na furaha na wakati wapekee waninyi kujumika
pamoja. Nahatakama mahusiano yako yanaonekana kuwa magumu wewe fikiri
namna ya kuyarejesha.
Chukulianeni kwa nidhamu/heshima.
Kumchukulia mpenzi wako kwa heshima kutwasaidia kuwa na mahusiano ya kudumu na yafuraha.
Mfanyie mpenzi wako vile wewe unavyo itaji kufanyiwa.
- Shiriki na mwenzako katika kufikiri mambo yamsingi , kama uzazi, namambo yamsingi kwa pamoja.
- Kubalianeni kwapamoja kabla yakufanya mipango.
- Mjulie mwenzoko juu ya kazi, anapenda nini, shughuli, na hisia.
- Epuka kumuita jina au tabia ambayo itamdhalilisha mpenzi wako.
Kuwa mwaminifu.
Kunatofauti yakuwa mkweli na kuwa muaminifu. Wapenzi ambao niwaaminifu
kwakila mmoja wanafurahiya mahusiano ya kudumu kuliko wengine. Tabia
yakutokuwa muaminifu kwa mpenzi wako kunaweza kuletamadhara makubwa sana
kwenye maisha yako hata kuliko kuaribu mahusiano yako ty!
Kuwa na muda wakufurahi pamoja.
Kwaujuma inakuza mahusiano, Tunakuwa busy kwashughuli za maisha hivyo
ukipata muda wakukaa na mpenzi wako unafahamu mengi kutoka kwake na
kufurahia uwepo wake kwaku share mwazo na hisia. Kumbuka kuwa na muda wa
pamoja bila kuingiliwa na mitandao ya kijamii, watoto, marafiki, ndugu,
jamaa na hata wazazi au shughuli za kazi. Mkiwa pamoja epuka kutumia
simu kuwa busy na mitandao ya kijamii.
Kuwa na muda wa kufurahi mwenyewe.
Wakati kuwa na muda wa kufurahi pamoja kunasaidia kukuza mahusiano ya
kudumu na furaha, Pia kwaupande wakuwa na muda wakufurahi mwenyewe
kunaongeza penzi lenu kudumu na furaha. Unapata muda wa kujipumzisha na
kupeana muda wa kum-miss mwenzako nakuwa na shauku ya kuwa naye tena
pamoja.
Usiruhusu wengine waingilie mahusiano yenu.
Binamu akiwa hana raha, wazazi, boss au rafiki juu ya mahusiano yeko
ambayo mnayajenga hiyo haikuhusu maan ahapo ni hisia zako na sio zao.
Labda kama wameona ukisalitiwa nasio kwa namna nyingine. Kama upo na
furaha juu ya mahusiano yako basi dumisha.
SULUHISHA MATATIZO.
Usitake kushinda mzozo.
Usiwe mtu wakutaka kushindana pale kunapokuwa na mzozo ili ushinde
nakuthibitisha upo sahihi. Tabia hii itakusababisha ushindwe kufikia
mafanikio maana hutakuwa sahih kwa kila jambo na mwisho wasiku kupoteza
penzi lako.
Kubali kuwa umefanya kosa.
Nikawaida kufanya kosa kwabinadamu yoyote yule ulimwenguni hata awe kiongozi wa dini, Kwanini isiwe kwenye mahusiano!
Lakini kwakukataa kukiri kosa ulilolifanya wakati umemuumiza mwenzio
haitakusaidia kwa wewe kuwa na mahusiano ya muda mrefu zaidi ya
mumupotezea muda.
Jaribu kusamehe.
Kushikilia kosa na kutotaka kuliacha liende zake kutakuumiza hatakama
ukiachana na mtu huyo. Kuwa na tabia ya kusamehe pale unapoombwa
masamaha na kusahau kisha kuanza mwanzo mpya bila kuwa na kumbukumbu ya
makosa yaliyo tokea.
Tafuta msaada.
Usiruhusu watu kiingilia penzi lako, Lakini ruhusu kupata msaada wa
mawazo na ushauri kisha unaupima utakuwa na manufaa mazuri kiasi gani
kwenye maisha yako na maendeleo ya mpenzi wako. Unaweza kupata ushauri
kwa wataalamu wamambo ya mahusiano, mtu mwenye hekima kama wazazi na
hata marafiki ambao wanafurahia furaha yako na mpenzi wako. Elewa
ukipewa ushauri na mtu ambaye anachukia upande mmoja wa mahusiano yako
basi usauri wako utakuwa mbaya.

Post a Comment