
Taasisi
1,200 duniani zitampa aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema,
Edward Lowassa Tuzo ya Amani kutokana na utulivu aliouonyesha kabla na
baada ya Uchaguzi Mkuu.
Akizungumza
kutoka Bukavu, DR Congo, mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, Amani na Haki
za Binadamu kwa jamii, Mchungaji William Mwamalanga alisema Lowassa
amechaguliwa jana mjini Bukavu na wajumbe 1,400 wa mkutano huo.
Mwamalanga
alisema wajumbe wanaohudhuria kongamano la amani wanatoka mataifa ya
Ulaya, Marekani, Asia na Afrika kwa kuwashindanisha wanasiasa 1,000 ili
kumpata Kiongozi Bora wa Amani mwaka 2015, ambaye anajali na kuangalia
maslahi ya jamii badala ya madaraka.
Hatua
ya kumpatia tuzo Lowassa ni baada ya kuelezwa kuwa amedumisha amani
hiyo hata baada ya kushindwa uchaguzi Mkuu wa Rais Oktoba 25.
Katika
uchaguzi uliopita, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)ilimtangaza Dk John
Magufuli kuwa mshindi kwa kupata kura 8,882,935 ikiwa ni asilimia 58.46
wakati Lowassa alipata kura 6,072,848 sawa na asilimia 39.97 ya kura
zote.
Mchungaji
Mwamalanga alisema katika kongamano hilo, wajumbe walijadili hali ya
amani duniani na mchango wa wanasiasa katika kulinda amani hiyo.
Alisema
kuwa wanasiasa barani Afrika wamekuwa vyanzo vya migogoro na mauaji ya
raia wakati wa uchaguzi, kama ilivyo nchini Burundi. Hata hivyo, alisema
kuwa wajumbe walipongeza ushindi wa Dk Magufuli, lakini wakasema
umetiwa dosari na hali ya kisiasa Zanzibar baada ya matokeo kufutwa.
Alisema
wajumbe wa kongamano hilo linaloshirikisha maaskofu, masheikh na vijana
kutoka madhehebu mbalimbali ya dini barani Afrika, wamemuhimiza Rais
Magufuli kumaliza utata wa uchaguzi wa Zanzibar.
Baada
ya kupitishwa kugombea urais kwa tiketi ya Chadema, Lowassa alitangaza
kuwa angefanya kampeni kistaarabu na kwa amani na baada ya matokeo
aliwatuliza wafuasi wa chama hicho, akisema “hakuna anayeweza kuizuia
bahati ya mtu” kwa hiyo kama amepangiwa kuwa rais, atakuwa.
Lowassa,
ambaye ni Waziri Mkuu wa kwanza wa Serikali ya Awamu ya Nne, aliongeza
upinzani kwenye uchaguzi wa mwaka huu baada ya kuihama CCM na kujiunga
na Chadema iliyoukuwa na nguvu ya vyama vingine vitatu vya NLD, CUF na
NCCR-Mageuzi.
Kama
alivyoahidi, Lowassa hakutumia mikutano yake ya kampeni kushambulia
mambo binafsi ya wagombea wengine, bali muda mfupi kuomba kura.
Post a Comment