MSANII Vanessa Mdee ambaye ni mmoja wa wanamuziki wanaoshiriki onyesho la Coke Studio linaloendel...
MSANII Vanessa Mdee ambaye ni mmoja wa wanamuziki wanaoshiriki onyesho
la Coke Studio linaloendelea, amewaasa wanamuziki wa Tanzania kufanya
kazi kwa bidi na kuzingatia falsafa ya ‘hapa kazi tu’ iliyoanzishwa na
Rais wa Awamu ya Tano wa Tanzania, John Magufuli.
Akizungumza na vijana juu ya mafanikio yake jijini Dar es Salaam jana, Vanessa alisema kuwa mafanikio aliyonayo hayakuja kama mvua, bali yametokana na kufanya kazi kwa bidii, kujiamini na kuwa mbunifu.
“Mafanikio yoyote yanataka kujituma, hivyo ni muhimu kwa wasanii wachanga na wakongwe kufanya kazi kwa bidii zaidi ili wapate mafanikio na nawahakikishia kuwa kazi ya muziki inalipa na inaweza kutoa ajira kwa vijana wengi,” alisema Vanessa.

Post a Comment