Featured

Loading...


Ziara ya Lowassa Nchi Nzima 'Yaota Mbawa' Ghafla......CHADEMA Watoa Ufafanuzi


Siku moja baada ya kuahirishwa ziara ya aliyekuwa mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, chama hicho kimesema hakilitambui zuio la kufanya maandamano na mikutano ya kisiasa lililowahi kutolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali (IGP) Ernest Mangu mwezi uliopita.

Kauli ya Chadema ilitolewa jana na Ofisa Habari wa chama hicho, Tumaini Makene, baada ya kuulizwa juu ya kuwapo taarifa kuwa wameshindwa kuendelea na ziara ya Lowassa kutokana na zuio hilo.

Akizungumza Dar es Salaam jana, baada ya kuahirishwa mkutano na waandishi wa habari, Makene alisema katazo hilo la mikutano ya hadhara linaendelea.

“Hatulitambui tamko la IGP, sisi tuliahirisha kutokana na kutingwa na shughuli za uchaguzi mdogo, hivyo tukimaliza kushughulikia masuala hayo ya uchaguzi, tutarudi kuendelea na ziara kama tulivyopanga nchi nzima. Hata kama IGP kakataza, mbona CCM wanafanya mikutano ya hadhara?” alisema Makene.

Akizungumzia sababu za kuahirisha mkutano ambao chama hicho kiliuitisha jana na kusababisha waandishi wa habari kusubiri kwa zaidi ya saa tatu, Makene alisema kuna masuala ya msingi ambayo yalijitokeza katika suala la umeya wa Jiji la Dar Salaam ambalo ndilo lilikuwa ajenda.

“Tumeahirisha kwa sababu kuna figisufigisu tumefanyiwa kwenye umeya, hivyo tunazifanyia kazi,” alisema Makene.

Alisema lengo la kuita waandishi wa habari ilikuwa ni kutangaza jina la mgombea wa nafasi hiyo ya umeya wa Jiji la Dar es Salaam.

Mkutano wa viongozi hao ulikuwa ukiendelea ndani ya ofisi za chama hicho, huku kila mara baadhi ya viongozi wakitoka na kutoa matumaini kwa waandishi kuwa mkutano wao utaanza punde.

Mwezi uliopita, Jeshi la Polisi kupitia msemaji wake Advera Bulimba, lilipiga marufuku maandamano na mikutano kutokana na kudai kuwa tathimini iliyofanyika ilionyesha bado kuna mihemuko ya kisiasa ambayo itasababisha uvunjifu wa amani.

TOA MAONI YAKO HPO CHN1 KUHUSU HABARI HII

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright JICHO LETU
Back To Top