Makamu
mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein amesema kuwa miaka 39
ya kuzaliwa kwa CCM ni kilele tosha cha kupatikana kwa maendeleo katika
Nyanja mbali mbali za kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Akizungumza katika uziunduzi wa miaka 39 ya kuzaliwa kwa chama hicho katika viwanja vya Afisi kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar, amesema kuwa maendeleo yaliyopatikana katika serikali zote mbili ya Tanzania bara na Zanzibar yamesimamiwa na miongozo, ilani na mikakati mbali mbali iliyotokana na CCM.
Dkt.
Shein alisema kuwa CCM ilizaliwa mwaka 1977 baada ya kuungana kwa vyama
viwili vya ukombozi vikiwemo TANU na Afro shraz party (ASP) ambapo
chama hicho kimeweza kupigania haki za wanyonge kwa kusimasmisha
serikali zenye misingi imara ya kuwatumikia wananchi kwa moyo wote bila
ya ubaguzi.
“
Serikali nyingi zilizoundwa na vyama vya ukombozi duniani zimeangushwa
na wakoloni kwa njia za kitapeli lakini sisi serikali zetu bado ni imara
na zitaendelea kutawala wananchi kwa njia bora na za kidemokrasia.
"Pia
ni lazima tuendelee kujitathimini kwa kila jambo nje na ndani ya chama
chetu kwani bado kuna changamoto mbali mbali zinazotakiwa kufanyiwa kazi
ipasavyo”, alisema Dkt. Shein.
Aidha
Dkt. Shein aliwasihi wafuasi wa chama hicho na wananchi kwa ujumla
kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa marudio utakaofanyika Machi 20
mwaka huu, ili wapatikane viongozi wa kuongoza dola kwa mniaka mitano
ijayo.
Dkt.Shein
alifafanua kwamba msingi wa uchaguzi wa marudio upo kikatiba kwani
uchaguzi mkuu uliopita ulifutwa kisheria na mamlaka iliyokuwa inahusika
na usimamizi na uratibu wa uchaguzi huo baada ya kubaini kasoro.
Akizungumzia
mgogoro wa kisiasa uliopo visiwani Zanzibar, Dkt. Shein alisema kuwa
ulikuwa utatuliwe kwa njia za mazungumzo lakini kiongozi wa CUF ambaye
ni Maalim Seif Sharif Hamad aliyeomba mazungumzo ya maridhiano kabla
hayajamalizika yeye alienda kutoa siri za vikao kwa waandishi wa habari
Dar es saalam na baadae kuandika barua ya kujitoa katika mazungumzo
hayo.
Aidha
aliwataka wananchi kuendelea kulinda Amani na utulivu wa nchi na
kuepuka kutumiwa na baadhi ya vyama vya kisiasa kufanya vurugu
sizisokuwa na msingi kwa maslahi ya nchi.
Akizungumza
katika hafla hiyo Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai
alisema kuwa Zanzibar CCM itaendelea kuwa chama cha wananchi wote
kinachoongozwa na uzalendo.
Alisema
kuwa mpaka sasa CCM Zanzibar imejiandaa kwa kila hatua katika kushiriki
kwenye uchaguzi wa marudio utakaofanyika Machi 20 mwaka huu.
Post a Comment