Hakimu
Mkazi Mwandamizi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Said Mkasiwa
amekataa kujitoa katika kesi ya kulawiti na kutuma picha kwenye mitandao
ya kijamii inayowakabili washitakiwa Erick Kassira (39) na Juma Richard
(31).
Mkasiwa
alisema sababu zilizotolewa na washitakiwa hao kwamba wanatishwa na
kulazimishwa kesi isikilizwe wakiwa wanaumwa, si za kisheria ambazo
zitamfanya asiendelee kusikiliza shauri hilo.
Wakitoa
pingamizi jana, washitakiwa hao walidai kuwa hakimu huyo anawalazimisha
kusikiliza kesi wakiwa wanaumwa na kwamba anawakataa wadhamini ambao
washitakiwa hao waliwapeleka mahakamani hapo.
Mshitakiwa
Kassira alidai kuwa Januari 4, mwaka huu alimuandikia barua Hakimu huyo
kumuomba asiendelee kusikiliza kesi hiyo, badala yake achague mwingine
atakayeweza kusikiliza.
Alidai kuwa hawana imani na hakimu huyo kwa kuwa anawapendelea zaidi upande wa mashitaka na kushindwa kuwasikiliza.
Hata
hivyo, Hakimu huyo aliwaeleza washitakiwa hao kuwa sababu walizozitoa
sio za kisheria na kwamba ataendelea kusikiliza shauri hilo.
Wakati
huo huo, shahidi wa tano katika kesi hiyo, Tegemea Chaula (52), mkazi
wa Kiwalani na mhudumu wa nyumba ya kulala wageni ya Maembe iliyopo
Yombo Kiwalani, alidai kuwa mlalamikaji alifika katika nyumba hiyo na
kuulizia kama vyumba vipo.
Chaula
alidai kuwa, Agosti 23, mwaka 2014 mlalamikaji aliingia saa 7:00 mchana
ambapo alipatiwa chumba namba sita pamoja na funguo.
Akiongozwa
na Wakili wa Serikali, Sylvia Mitanto, shahidi huyo alieleza kuwa
anamfahamu mlalamikaji kwa muda mrefu kama mshauri wa masuala ya Ukimwi
na kwamba alikuwa anapeleka wateja katika nyumba hiyo ya kulala wageni.
Alidai
saa 12:00 jioni alimuona mlalamikaji akiwa katika mlango wa kutokea
akiwa amevaa shati na taulo huku akiwa hajavaa viatu.
“Aliniita
na kuniulizia Meneja wa gesti hii, Mohamed Hamza, nilimuita na
kuongozana kwa pamoja kwenda chumbani kwa mlalamikaji ambapo alikuwa
anaonekana hana furaha,’’ alidai Chaula.
Post a Comment