RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekutana
na kufanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
Dkt. Richard Sezibera Ikulu Jijini Dar es Salaam, ambapo pamoja na mambo
mengine Rais Magufuli amepokea taarifa ya maandalizi ya Mkutano wa
Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika tarehe 02
Machi, 2016 Katika Jiji la Arusha, Nchini Tanzania.
Rais
Magufuli ndiye Mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
inayojumuisha nchi tano wanachama ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda,
Rwanda na Burundi.
Akizungumza
mara baada ya mazungumzo hayo Katibu Mtendaji wa Jumuiya hiyo Dkt.
Richard Sezibera, amesema maandalizi kuhusiana na mkutano huo yanakwenda
vizuri.
Amesema
pamoja na mambo mengine mkutano huo, utajadili masuala kadhaa yakiwemo
mpango wa kuanzisha viwanda vya magari ndani ya Jumuiya ili kupunguza
uingizaji wa magari kutoka nje ya nchi na Marais kuzindua pasi ya
kusafiria ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kuhusu
hali ya Jumuiya, Dkt. Sezibera amesema inaendelea vizuri na ametaja
baadhi ya mambo ambayo yamefanyika kuwa ni kutiwa saini kwa mkataba wa
umoja wa forodha, makubaliano ya soko la pamoja na makubaliano ya sarafu
moja.
Mengine
ni kuwepo kwa mazungumzo kuhusu uimarishaji wa miundombinu kama vile
reli na umeme ndani ya Jumuiya, na mazungumzo kuhusu umoja wa kisiasa.
Kwa
upande wake Waziri wa Mambo ya nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Kikanda na Kimataifa Dkt. Augustine Mahiga, amesema Tanzania ikiwa ni
mwenyeji wa kikao hicho ipo tayari kupokea ugeni na kwamba pamoja na
kufanyika kwa kikao hicho, marais wa Tanzania na Kenya watafungua
barabara inayounganisha Tanzania na Kenya katika Mpaka wa Holili na
kutakuwa na shughuli ya kuweka jiwe la msingi katika kituo cha pamoja
cha mpakani kwa ajili ya kuwezesha upitaji wa mizigo na watu yaani "One
Stop Boarder Post"
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es salaam.
24 Februari, 2016.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza na Dkt. Richard Sezibera, Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki Ikulu jijini Dar es Salaam Februari 24,2015
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiagana na Dkt. Richard Sezibera, Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki Ikulu jijini Dar es Salaam Februari 24,2015 baada ya
mazungumzo
Post a Comment