Mamlaka
ya mapato nchini (TRA) imeibukia tena Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) lakini safari hii haijapiga kufuli account za TFF badala
yake imeondoka na magari matano yanayomilikiwa na shirikisho hilo
kutokana na kulidai kiasi kikubwa cha kodi.
TRA
imeamua kuchukua magari hayo ikitaka TFF kulipa deni la malimbikizo ya
kodi mbalimbali wanayodaiwa ili warejeshewe magari yao.
Richard
Kayombo ni afisa wa TRA amethibitisha kuyakamata magari hayo
yanayomilikiwa na TFF lakini amefafanua sababu zilizopelekea kufanya
hivyo.
“Ni
kweli tumekamata magari matano ya TFF na hayo magari yamekamatwa kama
sehemu ya mwendelezo wa kuweza kupata mapato yanayotokana na deni la
kodi ambalo TFF hawajalipa.
“Mpaka
sasa tunawadai billion 1.118 ambayo ni kodi mchanganyiko kuanzia mwaka
2010 hadi 2015. Ikumbukwe hapo nyuma tulikamata account zao kwasababu
deni lilikuwa ni billion 1.6 na tukaweza kupunguza sehemu ya deni lakini
bado halijaisha na ndiyo sababu ya kukamata hayo magari matano.”
Hii
ni mara ya pili kwa TFF kupigiwa hodi na TRA ikilalamikiwa kulimbikiza
madeni ya kodi, mara ya kwanza TRA ilizifunga account zote za TFF lakini
safari hii wameamua kuyashikilia magari yao.
Kwa
mujibu wa Kayombo, magari hayo yapo kwenye yard ya YONO likiwemo basi
ambalo hutumiwa kuisafirisha timu ya taifa ‘Taifa Stars’.
Post a Comment