Uchambuzi wa magazeti leo 25 September 2015 umesikika moja kwa moja kutoka @CloudsFM ‘The Peoples Station’, na kama kawaida ripota wako wa nguvu anazo zile zote kubwa za leo kwenye kurasa za magazeti.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi Celina Kombani afariki dunia jana nchini India alipokuwa anapata matibabu, Mahujaji 117 wapoteza maisha Mecca, matokeo ya utafiti wa TWAWEZA yaendelea kupingwa huku UKAWA wasema utafiti huo umelenga kuibeba CCM, James Mbatia ametoa mualiko kwa TWAWEZA katika mdahalo huru ili kujibu maswali yaliokosa majibu kuhusu utafiti huo.
Kampuni ya IPSOS
imekana ripoti iliosambaa jana ikielezea matokeo yake ya utafiti wa hali
ya kisiasa nchini huku utafiti huo ulionyesha kuwa kama Uchaguzi mkuu
ungefanyika mwezi September Mgombea Urais CCM John Magufuli angeshinda kwa 62% na Mgombea Urais CHADEMA Edward Lowassa angeshinda kwa 31% na Mgombea Urais kupitia ACT Wazalendo Anna Mgwila 0.3%.
Mgombea Urais CHADEMA Edward Lowassa
asema hatakubali kushindwa mpaka pale itakapo bainika kuwa Uchaguzi
Mkuu ulifanyika kwa haki na taratibu zote zilifuatwa bila wizi wa kura, Rais Jakaya Kikwete amesema hamshangai mgombea Urais kupitia chama chake Dk. John Magufuli kukosoa utendaji kazi wa Serikali yake katika kampeni zake, asema yuko sawa kwani kila kiongozi ana namna yake ya kuongoza.
Waangalizi wa Umoja wa Ulaya EU wanaendelea kuwasili nchini, Maafisa polisi nchini South Africa wanamshikilia mwanaume mmoja kutoka Ujerumani aliyekamatwa kwa madai ya kuhifadhi sehemu za siri 21 za wanawake kwenye jokofu, upelelze juu yake bado unaendelea.
Nimekuwekea sauti yote ya uchambuzi wote wa magazeti kwenye #PowerBreakfast hapa chini.


Post a Comment