Featured

Loading...


Mahakama yamwamuru Gwajima kuthibitisha kama kweli anaumwa


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemwamuru Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima awasilishe Mahakamani hapo vyeti vinavyoonesha kuwa  ni mgonjwa.

Amri hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Cyprian Mkeha baada ya Gwajima kushindwa kufika mahakamani kwa ajili  ya usikilizwaji wa kesi inayomkabili.

Gwajima anakabiliwa na kesi ya kutumia lugha chafu dhidi ya Akofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinal Pengo.

Kesi hiyo ambayo tayari imeshaanza kusikilizwa ilitarajiwa kuendelea kusikilizwa mahakamani hapo ambapo upande wa mashtaka ulitarajiwa kuwasilisha kielelezo cha ushahidi ambacho ni mkanda wa video unaodaiwa kumwonesha Gwajima akitoa lugha hiyo chafu dhidi ya Kardinal Pengo.

Hata hivyo Gwajima hakutokea mahakamani na badala yake, Wakili wake Peter Kibatala aliieleza mahakama kuwa mteja wake hakuweza kufika mahakamani kwa kuwa anaumwa. Hata hivyo haikuweza kubainishwa kuwa Gwajima anaumwa nini.

Wakili wa Serikali Lilian Itemba aliiomba mahakama iagize mshtakiwa huyo awasilishe mahakamani vyeti vinavyothibitisha kuwa anaumwa.

Hakimu Mkeha alikubaliana na ombi hilo la upande wa Serikali na kuamuru mshtakiwa huyo awasilishe mahakamani hapo vyeti hivyo, siku ya tarehe ya kuendelea kwa usikilizwaji wa kesi hiyo.Hakimu Mkeha aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 4, 2015.

TOA MAONI YAKO HPO CHN1 KUHUSU HABARI HII

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright JICHO LETU
Back To Top