Featured

Loading...


Waziri Mkuu Mizengo Pinda Awapigia Magoti Watanzania..Adai Wamsamehe Kwa Matamshi Aliyoyatoa Wakati Akiwa Kiongozi

Waziri Mkuu Mizengo Pinda, jana alitumia Ibada ya Shukrani iliyofanyika katika Parokia ya Hananasifu, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, kumshukuru Mungu kwa kumwezesha kulitumikia Taifa kwa zaidi ya miaka 15 na kuwaomba Watanzania wamsamehe kwa matamshi aliyoyatoa akiwa kiongozi, huenda yaliwakwaza baadhi yao.

Pinda ambaye amekuwa Waziri Mkuu kwa miaka minane na miezi tisa, Waziri kwa miaka miwili na nusu na Naibu Waziri kwa miaka mitano, alisema anasikia fahari kumaliza uongozi wake kwa furaha na amani.

Moja ya kauli tata zilizowahi kutolewa na kiongozi huyo iliyozua sintofahamu ni ile ya Juni 29, 2013 katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma alipoviagiza vyombo vya dola kuwashughulikia kwa kuwapiga wale watakaokataa kutii amri wakati wakifanya vitendo vya uvunjifu wa amani.
Kauli nyingine tata ni ile ya mwaka 2009 baada ya kuwaeleza wanaoua watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) pamoja na vikongwe hawana budi kuuawa kwa kuwa wakisubiri mahakama kuwahukumu, watakuwa wanakosea.

Katika ibada hii ya shukrani, nimemuomba Mungu anisamehe kwa matamshi niliyoyatoa nikiwa kiongozi yanaweza kuwa yaliwaudhi watu bila mimi kujua. 
“Uwaziri Mkuu ni kazi ngumu yenye changamoto nyingi. Nitakuwa mtu wa ajabu nisipomshukuru Mungu kwa uongozi wake katika kipindi chote hicho tangu nikiwa naibu waziri hadi kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu,” alisema.

Pinda alisema katika utumishi wake kwa umma amejifunza mambo mengi lakini kikubwa zaidi ni kujua jinsi ya kuishi na watu.
Katika hatua nyingine, Abate Thadei Mhagama wa Abasia ya Hanga, aliwataka waumini nchini wazidishe maombi kwa kufunga na kuomba kwa siku sita zilizobaki kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu.

Ninawaomba waumini wote tuzidishe sala ili nchi iendelee kuwa na amani na upendo, tumwombe Mungu pia atuwezeshe kupata viongozi aliowandaa kwa yeye kwa maana ya rais, wabunge na madiwani,” alisema Mhagama.
Alisema uchaguzi wa mwaka huu ni wa aina yake kwani demokrasia imekuwa miongoni mwa Watanzania.

Sote ni mashahidi, tumeona kwenye mikutano kila mgombea akija sote tunajaa huko. Hii ni kwa sababu hatujui yupi ni yupi, ndiyo maana nasisitiza kuwa tumuombe Mungu atuletee yule ambaye amemuandaa yeye,” alisisitiza.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Baraza la Walei katika parokia hiyo, Arbogasti Warioba alisema:

“Sote tunatambua kuwa kazi aliyoifanya Waziri Mkuu Pinda ilikuwa ngumu, misafara ilikuwa ni mingi na wakati mwingine ilikuwa ya mwendo mkali, lakini Mungu alimtetea na kumlinda hadi leo yuko salama.

  "Tunakushukuru pia kwa ushirikiano ulioendelea kutuonyesha wakati ukiwa madarakani na tunakuombea uendelee kuwa na ucha Mungu katika maisha yako ya uraiani.”

Source: Mpekuzi blog

TOA MAONI YAKO HPO CHN1 KUHUSU HABARI HII

KAMA UMEGUSWA NA HABARI ZETU ...BASI BOFYA LIKE HPO CHINI KUUNGANA NASI KWENYE FACEBOOK

During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:.;

Post a Comment

CodeNirvana
© Copyright JICHO LETU
Back To Top