Wadaiwa
16 waliokwepa kulipa kodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), baada ya
kutorosha kontena za mizigo yao kwenye Bandari Kavu (ICD) ya Azam
mwishoni mwa mwaka jana, mali zao zinaanza kukamatwa leo na kufilisiwa.
Mkurugenzi
wa Mtendaji wa Kampuni ya Udalali ya Yono, iliyopewa kazi ya kufuatilia
wadaiwa hao wakiwemo baadhi ambao wamekamilisha malipo, Yono Kevella
alisema hayo Dar es Salaam jana.
Kevela
alisema kuanzia leo wanakaa na vyombo vya dola, kuanza utaratibu wa
kukamata na kufilisi mali za wahusika na kuwafikisha kwenye vyombo vya
sheria.
Kevela
alisema hadi sasa hakuna zuio lililotolewa, linazowazuia kutekeleza
wajibu wao katika kukusanya madeni hayo. Hata hivyo alisema, wengi wa
wadaiwa baada ya kutolewa kwa muda huo wa siku 14, wameonesha moyo wa
kulipa.
Wadaiwa 16 hawajamaliza madeni
Alitaja
wadaiwa 16 ambao hawajalipa madeni yao wala kupunguza, ambao
watafilisiwa wasipojitokeza kufanya malipo ni Said Ahmed Said Sh
28,249,352.50, Strauss International (45,393,769.95), Farid Abdallah
Salum (52,185, 614.97).
Wengine
ni Nasir Saleh Mazrui (60,105,873.77), Simbo Yona Kimaro
(64,221,009.10), Ally Masoud Dama (102,586,719.22) na Juma Kassem Abdul
(130,182,395.12), Salum Link Tyres (233,447,913.31) na Tybat Trading
Co.Ltd (448,690,271.90).
Pia
wamo IPS Roofing Co.Ltd (966,723,692.10), Tuff Tyres General Co Ltd,
(7,435,254,537.03), Swalehe Mohamed Swalehe (34,687,165.00), Rushwheel
Tyre General Co Ltd, (1,802,988,679.20), Said Ahmad Hamdan
(68,362,558.31), Ahmed Saleh Tawred ( 59,237,578.40) na Farida Abdullah
Salem Sh 75,334,871. 85.
Akizungumzia
wadaiwa waliolipa ndani ya siku 14 walizopewa na zikaisha juzi, alisema
wanane kati ya 24, ndiyo walijitokeza kulipa madeni baada ya kampuni
yake kuwafuatilia.
Kevela alisema hadi jana zaidi ya Sh milioni 200 zimelipwa na wadaiwa hao.
Wadaiwa
hao 24 walishindwa kulipa kodi kwa wakati kama walivyotakiwa kufanya,
ndipo TRA ilimpa dalali huyo kazi ya kuwafilisi. Kampuni hiyo ya udalali
ilitoa siku 14, kuanzia Februari 10, mwaka huu wawe wamekamilisha; muda
ambao umeisha juzi.
Kevela
alisema katika siku hizo 14, kati waliojitokeza kulipa,wanne kati yao
wamemaliza madeni na wengine wanne wamepunguza madeni na kuahidi
kumalizia kiasi kilichobaki.
Waliomaliza madeni yao
Wadaiwa
waliolipa madeni yao yote ni Issa Ali Salim aliyekuwa akidaiwa Sh
94,543,161.96, Libas Fashion (26,593,245.78), Omary Hussein Badawy
(21,346,615.40) na Zulea Abas Ali (16,760577.24).
Waliopunguza madeni yao
Waliopunguza
madeni yao ni Zuleha Abbas Alli aliyelipa Sh milioni 47 na kubakiwa na
deni la Sh 28,508,551, awali alikuwa akidaiwa Sh 75,508,551.88, mwingine
ni Ally Awes Hamdani aliyelipa Sh milioni 17.26 awali alikuwa akidaiwa
Sh 55,485,904.07).
Wengine
waliopunguza kidogo ni Tifo Global Trading Co Ltd waliolipa Sh milioni
mbili ilhali deni lao ni Sh 1,573,300,644.58, Lotai Steel Tanzania Ltd,
waliolipa Sh milioni mbili ilhali deni lao ni Sh 5,476,475,738.19.
“Tulikabidhiwa
wadaiwa 24 na TRA, waliokwepa kodi kwa kutorosha kontena katika bandari
kavu ya Azam mwishoni mwa mwaka jana, sasa walipewa muda wa kulipa ila
walikaidi, tukakabidhiwa tuwafilisi mali zao zote ili kulipia madeni na
wamejitokeza hao na kuanza kulipa wengine wamemaliza”, alisema Kevela.
Awali
wadaiwa 24, walikwepa kodi ya Sh bilioni 18.95 kwa kutorosha makontena
329 ya bidhaa zao kutoka Kampuni ya SSB ambayo ndiyo mmiliki wa bandari
kavu ya (Azam ICD) na kampuni ya Regional Cargo Services.
Mapema
Desemba mwaka jana aliyekuwa Kaimu Kamishna wa TRA, Dk Philip Mpango
alizungumza na waandishi wa habari na kusema kampuni 15 kati ya 43,
zilizokwepa kodi baada ya kutorosha kontena 329 katika ICD ya Azam,
wamelipa.
Dk
Mpango alisema Desemba 12, mwaka jana ndiyo ilikuwa siku ya mwisho
aliyotoa Rais John Magufuli ya siku saba kwa wakwepa kodi hao 43, kulipa
wenyewe kwa hiari, vinginevyo sheria zitachukua mkondo wake. Kufuatia
kauli hiyo ya Rais Magufuli, wadaiwa 15 walijitokeza na kulipa na
waliobaki hawakujitokeza kulipa.
Post a Comment