Wananchi
wilayani Kiteto mkoani Manyara wamejiandaa kumpokea kwa mabango
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ili kutoa ujumbe wa kuwakataa
baadhi ya viongozi wa wilaya kutokana na kukithiri kwa
migogoro ya ardhi.
Miongoni
mwa viongozi wanaotajwa kuwamo katika ujumbe huo ni Mkuu wa
Wilaya Kanali Samweli Nzoka, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Bosco
Ndunguru,Katibu Tawala (DAS) Nicodemus John pamoja na kamanda wa
Polisi wa Wilaya (OCD) George Katabazi.
Hata
hivyo DC Nzoka amepiga marufuku mwananchi yeyote kuandaa bango
lolote katika ziara hiyo ya Waziri Mkuu inayotarajiwa kufanyika
Februari 29 mwaka huu.
Akizungumza
katika kikao cha baraza la Madiwani jana,Nzoka alisema
hataruhusu kuandaliwa wala kuonyeshwa mabango hayo kwani ni
ishara ya vurugu na uvunjifu wa amani.
Mkuu
huyo wa Wilaya alisema anazo taarifa za kuwapo watu
walioandaliwa kutoka wilaya na mikoa ya jirani kwenda Kiteto
kuzomea baadhi ya viongozi wa Wilaya katika ziara hiyo.
Katika
ziara hiyo, Majaliwa atakutana na kuzungumza na viongozi
mbalimbali wakiwemo madiwani, wakuu wa idara na viongozi wa
mila wa jamii ya wafugaji
Waziri
mkuu anategemewa kutoa suluhisho la mgogoro wa ardhi kati ya
wakulima na wafugaji uliodumu kwa muda mrefu na kusababisha
mauaji
Post a Comment